13 August 2013

TUKIO LA PONDA LAWASHA MOTO
 •  BAKWATA YALAANI YATAKA SHILOGILE AJIUZULU
 • MATAMKO MAZITO YATOLEWA NA TAASISI NCHINI
 • AFANYIWA UPASUAJI,POLISI WAPIGANA VIKUMBO
 Na Waandishi Wetu
TUKIO la Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Waislamu Tanzania, ShekhePonda Issa Ponda, kujeruhiwa kwakitu kinachodhaniwa ni risasi limezidi kugusa hisia za Watanzania na taasisimbalimbali,huku lawama zikielekezwa kwa Jeshi la Polisikutokanakuhusishwa natukio hilo.Baraza Waislamu Tanzania (BAKWATA)lenyewe limeenda mbali zaidi kwa kuitakaSerikali iunde tume huru ya kuchunguzatukio hilo na endapo itabainika polisiwalihusika, basi jeshi hilo litapoteza imanikwa jamii ya waislamu

.Mbali na kutaka iundwe tume hiyo,BAKWATA imemtaka Kamanda wa Polisiwa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile,kujiuzulu wadhifa huo ili kupisha uchunguzihuru wa tukio hilo. Akizungumza na waandishi wa habari jana kwa niaba ya BAKWATA, ShekheMkuu wa Mkoa, Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim, alisema kitendo cha kupigwa kwa Shekhe Ponda, na kitu kinachodhaniwa
risasi kimewasikitisha kwani kibinadamu nijambo baya.“Shekhe Ponda si jambazi, walikuwa nauwezo wa kumkamata pasipo kumdhuru,”alisema Shekhe Salim na kusisitiza kwambaShekhe Ponda anafahamika nyumbani kwake, hivyo ilikuwa ni rahisi kumkamata.Alisisitiza kwamba BAKWATA hainauadui na Shekhe Ponda na wafuasi wake hadi ifi kie hatua wafurahishwe na kitendo alichofanyiwa. Alisema BAKWATA
inatofautiana kimtazamo na fi kra na Shekhe Ponda, lakini hawana uadui wowote.
Wasomi wa Kiislamu
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendajiwa Taasisi ya Wasomi wa Kiislamu (TAMPRO), Sadiki Gogo, alisemawanalaani vikali kitendo hicho na wametakatume huru iundwe ya kuchunguza tukiohilo na watakaobainika wachukuliwe hatuaza kisheria. Walikataa tume iliyoundwa na polisi kuchunguza tukio hilo.
ache kujichukulia sheria mkononi, kwani itasababisha wananchi kuiga tabia hiyo na matokeo yake taifa litaelekea kubaya.“Serikali isiwe mstari wa mbele kuvuruga amani na badala yake iwe mstari wa mbelekusikiliza matatizo ya Waislamu,” alisemana kuongeza; “Serikali ihakikishe alipo Shekhe Ponda, anakuwa katika hali ya
usalama, kwani hadi sasa kuna polisi wodini, hivyo haijulikani wapo kwa ajili gani.”
Watetezi wa haki za binadamu
Wakati huo huo, mashirika matanoyakiwemo ya kutetea haki za binadamu nchini ya THRD-Coalition, LHRC, SIKIKA,CPW na TAMWA, yamelaani tukio la kupigwa risasi Shekhe Ponda. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Onesmo Ole Ngurumwa, alisema wanalaani kitendo hicho ikiwa ni pamoja na tabia ya wananchi kujichukulia sheria mikononi, kwani ni kinyume cha sheria. Alisema wanafahamu wajibu wa Polisi ni kulinda raia na mali zao, kuwakamata washukiwa wa uhalifu kwa mujibu wa sheria, lakini wanalaani utaratibu uliotumika kutaka kumkamata Shekhe Ponda. Kuhusu tume iliyoundwa na Jeshi la Polisikuchunguza tukio hilo, alisema kwa uzoefu walionao hawana imani na tume hiyo, kwani Polisi ndio wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo, hivyo hawezi kujichunguza. Alisema wanatoa wito kwa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora ambayo kikatiba ina jukumu la kufuatilia tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua stahiki za kisheria.Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dkt. Hellen Kijo-Bisimba, alisema mtu yeyote hatakiwi kupigwa risasi kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na haki za binadamu. Akizungumza na gazeti hili jana alisema ametoa agizo ofisi yake ianze kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo. Alisema tume ya uchunguzi itakwenda mkoani Morogoro kulipotokea tukio hilo,ili kupata ukweli wa tukio hilo.
Ponda afanyiwa upasuaji Muhimbili
Kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, waandishi wetu wanaripoti kuwa hali ya Shekhe Ponda, inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa bega juzi. Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Almasi Jumaa, alisema Shekhe Ponda, bado yupo wodini na kwamba kipimo cha X-ray kinaonesha kuwa alivunjika mfupa mkubwa wa bega, lakini mifupa haikutawanyika. “Ni ngumu kuthibitisha jeraha limetokana na nini kwa sababu alifi ka akiwa amepatiwa matibabu ya awali japokuwa kidonda kilikuwa katika hali isiyokuwa nzuri,” alisema. Alipoulizwa kama yupo chini ya ulinzi, Jumaa alisema hayupo chini ya ulinzi kwa sababu hana pingu na ni mgonjwa wao kama ilivyo kwa wengine. Alipoulizwa ni kwa nini kuna polisi wodini walipolazwa Shekhe Ponda, alisema hawezi kujua kwani wao hiyo si kazi yao. Gazeti hili lilishuhudia askari kanzu wakiwa MOI, huku wengine wakipigana vikumbo kuingia wodini alikulazwa na kutoka alikolazwa Shekhe Ponda.
Kova anena Kwa upande wake Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman
Kova, alikiri kuwa Shekhe Ponda yupo chini ya ulinzi. Alisema Ponda alikuwa akitafutwa na Polisi baada ya kuvunja masharti ya kifungo cha nje na amri ya mahakama kwa kufanya mikutano Zanzibar na Morogoro.
Kamanda Kova alisema kukamatwa kwake kumefanikiwa baada ya kupata taarifa kuwa anapatiwa matibabu MOI.Alisema yupo chini ya ulinzi kwa ajili ya usalama wake.
Imeandikwa na Darlin Said, Rehema
Maigala, Kassim Mahege, Frank Monyo
na Theophan Ng’itu


6 comments:

 1. Makusudio ilikuwa ni kumuua na baadae kuubababaisha umma. Bahati nzuri Mungu amemwepusha na hilo hadi hapo ahadi yake itakapofika. Lakini wakumbuke makafiri wa serikali hii dhalimu ya kuwa wakimuua Ponda tutalipiza kisasi kwa askari kumi bila kupungua. Hiyo ni jihadi tunawatangazia.

  ReplyDelete
 2. Ni kweli huo ni mpango haramu wa polisi, lakini wasije wakaendelea nao mpango huo kwani madhara yatakayokuja ni makubwa kuliko wanavyodhani, sera hizi za kuwamaliza waislam lazima ziishe, tunawaona akina mtikila wakihutubu machafu mangapi ya ugombanishi lakini hakuna cha maana kinachofanyika lakini ikibidi ni muslam basi atamalizwa tu, sheikh kasim bin jumaa kila mtu anajua amepewa sumu kule jela, polisi mkifanya unyama kwa ponda tutawaonyesha, wale amabao hawajapata suna tutawatahiri na kuingiza clips zao kwenye internet

  ReplyDelete
 3. KAULI KUWA TANZANIA IAONGOZWA NA MAKAFIRI HAIKUBALIKI NIMESIKITISHWA NA MUFTI SIMBA KUNYAMAZIA KAULI ILIYOTOLEWA NA PROFESA LIPUMBA NA SHEHE WA DAR ES SALAAM IWAPO SERIKALI NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VIKILOGWA VIKAFANYA KAZI KISIASA YALE YANAYOTOKEA MISRI TUYASUBIRI PUNDE YATATOKEA TANZANIA

  ReplyDelete
 4. Kama analeta mambo ya Al Qaeda na auliwe maana hao ni wauaji. Mambo ya kupiga watu mawe hadi kufa kisa katenda kosa nani kamruhusu. Mungu gani yeye. Yeye amekuwa Mungu tangu lini. Si Nabii, Si Mtume bali ni JITU UAJILINALO TAFUTA UMAARUFU DUNIANI.
  Bora lingekufa kuliko kuja kuua watu bure. Tena jina Ponda? Lipondwe lenyewe. Watu wengi wafe kisa mtu mmoja ni sheria ya wapi.

  Apelekwe mahakamani akatolewe hukumu yake huko inayo mstahili. Mungu si mjinga, si kiziwi, si bubu, bali yupo na anaona matendo yetu maovu na masafi. Miaka yote tumeishi vema Waislamu na Wakristo hata hao makafiri lakini Amani ilikuwepo, aje yeye Ponda ndipo auponde upendo na amani iliyodumu miaka dahali? AJIREKEBISHE HATUTAKI AL QAEDA, WALA BOKO HARAMU WALA AL SHABAB nchini kwetu. Siyo lazima mtu awe muislam au mkiristo na hiari yake mtu, Pponda atuache.

  ReplyDelete
 5. Whatever PONDA has done, he deserves to live. Stop blessing the killings done by Tanzanian POLICE every now and then. I'm Christian, I love PONDA, I love my Country.

  ReplyDelete
 6. nina marafiki wengi waislam ,na wala hatuna shida haya mambo ya chuki tuachane nayo,kuna wasiopenda ,nchi yetu ilivyo nawiri tuwe makini sana tumezungukwa na majirani tusiowajua vizuri tupendane kwa ajili ya wajukuu na vitukuu vyetu tofauti zetu zisituletee maafa,na utawala wa sheria ufanye kazi I love Tanzania.

  ReplyDelete