13 August 2013

KESI YA PINDA YAPATA MAJAJI

 • WANAONGOZWA NA JAJI KIONGOZI


Na Rehema Mohamed
JAJI Kiongozi, Fakhi Jandu, anatarajiwa kuongoza jopo la majaji watatu watakaosikiliza kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) dhidi ya Waziri Mkuu,Mizengo Pinda

.Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,majaji wengine waliomo kwenye jopo hilo ni Jaji Augustine Mwarija na Dokta Fauz Twaib.Hata hivyo tarehe ya usikilizaji wa shauri hilo bado haijapangwa. LHRC na TLS walimfungulia Waziri Mkuu Pinda, kesi hiyo kutokana na kauli yake aliyoitoa bungeni ya kuruhusu vyombo vya usalama kuwapiga watu wanaokataa kutii sheria zinazotolewa na mamlaka husika.Mbali na Pinda, mwingine aliyeunganishwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambapo kwa upande wa LHRC inawakilishwa na mawakili zaidi ya 20.Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Waziri Pinda, anakabiliwa na tuhuma za kudaiwa
kuvunja Katiba ya nchi kwa kuruhusu askari kuwapiga wananchi.Mkurugenzi wa LHRC, Dkt. Hellen Kijo Bisimba wakati akifungua mashtaka hayo katika Mahakama Kuu alisema kuwa wanamshtaki Waziri Mkuu kwa maelezo kuwa amekiuka kifungu cha Katiba Ibara 13 (1).Pinda ametajwa kwenye hati hiyo akiwa mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo namba 24. Naye Mjumbe wa Bodi ya LHRC, Wakili Dkt. Ringo Tenga alisema katika kesi hiyo wameangalia zaidi sheria na hasa haki za msingi za binadamu na kwamba kauli hiyo ya Waziri Mkuu Pinda inahatarisha haki hizo.Hata hivyo, hatua hiyo ya LHRC ilipingwa
vikali na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Nchini (DPP), Dkt. Elieza Feleshi akisema hakuna uhalali wa mashtaka yoyote dhidi ya kiongozi huyo sababu kauli ya Pinda kuwa pigeni haikuwa piga ua.

4 comments:

 1. WATOKEZE WANZANIA WA KUISHITAKI TAASISI HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KWA KUFANYA KAZI KAMA CHAMA CHA SIASA NINA ZUNGUMZA HIVYO KUTOKANA NA MATUKIO MENGI YANAYOENDELEA YA WATANZANIA KUJERUHIWA KWA KUMWAGIWA ASIDI ,KUUAWA PADRI AMBROSI,KUAWA MABILLIONEA WAWILI WAKIONE KUWA SIO BINADAMU BALI BINADAMU NI SHEHE PONDA TAASISI HII NI YA KISIASA NA INA UDINI NI AFADHALI IFUTWE HATUNA IMANI NAYO KAMA INALIPWA KWA KODI ZA WATANZANIA IFUTILIWE MBALI INAIPELEKA NCHI JEHANAMU

  ReplyDelete
  Replies
  1. Acha ujinga wewe! Fikiri kama mtu mwenye akili timamu. Serikali imekuwa dahifu sana ndiyo maana uhalifu unazidi kuchukua kasi ya ajabu sana. Wote walioumizwa ni binadamu. Ni bora tukawashukuru na kuwaunga mkono au kuwatia moyo wale wanaojitokeza adharani kulaani vitendo hivyo vya kiharifu dhidi ya binadamu kuliko kuwalaumu. Nadhani umetumwa, au umekaririshwa au uko nyuma ya uharifu unaotokea. Jitathimini.

   Delete
 2. Nadhani Pinda alirukwa na akili kwa sababu ya kulewa madaraka. Viatu alivyovaa ni vikubwa sana. Ubongo wake ni mdogo sana kufikiri mambo makubwa ya kitaifa. Mwanasheria aliyesoma lakini hakuelewa anasomea kitu gani.
  Amepotza mwelekeo. Zero kabisa.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Aisee unjua mabezo wewe. Utadhani ilisomea Jamaika vile! Pinda fanya kazi. Serikali fanyeni kazi wazibitini wahuni hao. Tupo katika vita vya kifikra vijana wetu wanadanganywa na kumalizwa na wahuni mwisho watalizwa tu. Wanapewa ahadi nyingi za uongo kwavile hawajui watanzaia walikuwaje miaka hamsini iliyopita.

   Delete