Na
Ester Maongezi
KAMPUNI ya
'Hall of Sam B and Promotion Companies' wameandaa pambano la ngumi la dunia
uzito wa kati (WBF) kati ya bingwa wa bara la Afrika, Francis Cheka na Philly
William wa nchini Marekani litakalofanyika Agosti 30, katika ukumbi wa Diamond
Jubilee, Dar es Salaam
Akizungumza Dar es Salaam
jana Mratibu wa pambano hilo, Jay Msangi, alisema kuwa pambano hilo litakuwa ni
la raundi 12 na uzito wa kilo 76 pamoja na kusindikizwa na mapambano mengine
manne.Msangi alisema mbali na
pambano hilo pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kati ya Mada Maugo pamoja
na Thomas Mashali pambano la raundi 12.
Msangi alisema aliamua
kuwakutanisha Maugo na Mashali katika pambano la utangulizi ili kuweza kuvunja
majigambo kati ya mabondia hao wawili."Unajua Maugo na Mashali kila mmoja anajigamba
kuwa yeye ni bondia bora baada ya Cheka, yaani baada ya Cheka kushika nafasi ya
kwanza ya ubingwa wa Afrika wa pili ni wao hivyo swali la jibu hilo nani ni
nani litapatikana siku hiyo," alisema Msangi
Pia kutakuwa na pambano la uzito wa juu kati ya
Alphonce Mchumia na Deandre McCole wa Marekani, Ibrahimu Classic wa Tanzania
atakipiga na Simba wa Tundani wote wa Tanzania na kutakuwa na pambano kati ya
Cosmas Cheka na Allan Kamote.
Msangi alisema mpambano huo utukuwa wa kihistoria
nchini, hivyo amewataka mashabiki wa mchezo wa ngumi nchini kujitokeza kwa
wingi ili kujionea ushindani utakaojitokeza.Viingilio
katika pambano hilo litakuwa viti maalum ni sh.150,000, VIP gold 50,000 na
20,000 kwa viti vya kawaida.Tiketi zitaanza kuuzwa kuanzia keshokutwa huku
mgeni rasmi katika pambano hilo atakuwa Frankois Botha bingwa mara mbili wa
Dunia
No comments:
Post a Comment