02 August 2013

TISA MBARONI KWA KUCHAFUA CHANZO CHA MAJI Na Deogratius Chechele, Gairo
MAMLAKA ya Mji mdogo wa Gairo Wi l a y a n i G a i r o inawashikilia watu tisa kwa kosa la kuvamia na kuharibu chanzo cha maji baada ya kukutwa wakifyatua matofali na kufanya shughuli mbalimbali za kibinadamu katika maeneo hayo ambapo ni kinyume cha sheria ndogo za mamlaka hiyo.

Akithibitisha kukamatwa kwa watu hao Mkurugenzi wa Kampuni ya Inuka Group inayojiusisha na utunzaji wa mazingira katika mamlaka hiyo Elia Hiluka alisema kuwa watu hao walikutwa na kosa hilo baada ya kufanyika ukaguzi wa maeneo ya vyanzo vya maji na kuwakuta vijana hao wakiwa wanaendeleza shughuli za ufyatuaji wa matofali kwenye ukingo wa chanzo cha maji ndani ya mita sitini kinyume na sheria ndogo za hifadhi ya mazingira za mamlaka ya mji huo.
Hi l u k a a l i s ema k uwa kampuni yake kwa kushirikiana na mamlaka hiyo iliwataka wananchi wote wanaofanya shughuli za kuchafua na kuharibu chanzo cha maji katika eneo hilo kusitisha shughuli hizo kwani akipatikana na kosa hilo chini ya kifungu cha 11 cha sheria ndogo atatozwa faini ya shilingi 70,000 ya papo hapo na akikaidi atafikishwa mahakamani.
Aidha alisema kuwa kazi zote za kibinadamu katika vyanzo vya maji zinatakiwa kufanywa umbali wa mita sitini kutoka katika chanzo hicho ikiwa pamoja na ufugaji, ufyatuaji wa tofali na umwagaji wa taka ngumu na kemikali.
Kwa upande wake Kaimu mtendaji wa mamlaka hiyo, Victoria Komba aliwataka wananchi kuwajibika katika kulinda chanzo chochote cha maji kilichopo ndani ya eneo la mamlaka kwani nikosa kwa mtu yeyote kuchafua chanzo hicho.

No comments:

Post a Comment