Na Fatuma Rashid
WACHEZAJI wa timu ya Jeshi la Polisi
nchini inatarajia kuondoka leo, kwenda Namibia kushiriki mashindano ya nchi za
Kusini mwa Afrika (SARPCCO), yanayotarajiwa kuanza Agosti 16 mpaka 30, mwaka
huu.Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Utawala na Rasilimali wa Jeshi
la Polisi (DCP), Thobias Andengenye wakati wa makabidhiano ya bendera ya taifa
kwa wachezaji wa timu hiyo, alisema wachezaji hao wanatakiwa kuwa na nidhamu ya
kutosha ili kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania.
Mkuu huyo alisema wachezaji hao
wanakutana na watu kutoka nchi mbalimbali, ambao wana tabia tofauti ambapo kuna
mambo mengi yatakayojitokeza mabaya na mazuri, hivyo hawana budi kufuata yale
mazuri ili kujijengea sifa nzuri katika michezo."Ni watu wengi mtakaokutana nao
kutoka nchi mbalimbali zipatazo 14 na pia mtakutana na mambo mengi, ila
tunawaomba kuchukua yale ambayo mnajua yatailetea sifa nchi yetu,"
alisema.
Naye Ofisa wa Michezo wa Ukanda wa
Polisi, Damian Chonya alisema timu hiyo imejipanga Vizuri ambapo ilianza
mazoezi Julai 23, mwaka huu wakiwa chuoni hapo ila kwa wanariadha walikuwa
wakifanyia mazoezi Chuo cha Taaluma ya Sayansi ya Polisi kilichopo Moshi na
mpaka sasa, anaamini wachezaji wapo vizuri kwa ajili ya mashindano.
Chonya alisema michuano hiyo, ambayo
hufanyika kila baada ya miaka miwili, kwa mwaka huu timu hiyo inashiriki kwa
Mara ya tano, ambapo kwa mara ya kwanza walishiriki mwaka 2003 na waliweza
kufanya vizuri.Al i o n g e z a k uwa k a t i k a
michezo hiyo itakayoshirikisha nchi 14 za SARPCCO, lengo lake ni kuendeleza
umoja katika michezo.
Al i s ema wa l i h a k i k i s h a
wanashiriki semina zote za maandalizi zilizokuwa zikifanyika nchini Namibia,
ambapo semina ya kwanza ilifanyika Desemba mwaka jana, Aprili na ya mwisho
ilifanyika Julai mwaka huu. Timu hiyo itaondoka ikiwa na jumla ya watu 67,
ambapo kila timu itakuwa na viongozi wawili na wachezaji wa mpira wa miguu 21,
netiboli 14, riadha 18, vishale nane, mwandishi wa habari mmoja na daktari
mmoja
No comments:
Post a Comment