13 August 2013

SBL YAZINDUA KIBO GOLD Na Anneth Kagenda
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imefanya uzinduzi wa mwonekano mpya wa Bia ya Kibo inayosherehekewa kwa wingi mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro maarufu kama 'Kibo Gold'.Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo uliofanyika juzi katika Kiwanda hicho kilichopo mjini humo, Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji, Nandi Mwiyombella alisema bia ya Kibo Gold imekuwa ikitambulika kwa ubora na ladha nzuri kwa wateja.

"Ninaweza kusema kuwa, hivi sasa bia yetu ya Kibo inaangaza zaidi katika chupa ya kisasa kutokana na hivi tulivyofikia kileleni wadau wetu mbalimbali wameweza kushuhudia," alisema.Alisema, bia hiyo mpya ina mwonekano mpya wa chupa inayoashiria ubora wa kilichopo ndani ni yenye ubora ule ule wenye kiwango cha hali ya juu ila kwa chupa ya rangi ile ile iliyong'arishwa na shingo ndefu. Hata hivyo, alisema kuwa bia hiyo inazalishwa na Kiwanda cha Serengeti cha Moshi na inasambazwa mkoani hapo na mikoa jirani ya Arusha, Tanga na Manyara.

No comments:

Post a Comment