13 August 2013

SIMBA,3 PILLARS USO KWA USO KESHO Na Ester Maongezi
KIKOSI cha timu ya Simba, kesho kinatarajiwa kuteremka uwanjani kuvaana na 3Pillars ya Nigeria katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Wekundu hao wa Msimbazi Jumamosi katika uwanja huo, iliigagadua timu ya SC Villa ya Uganda mabao 4-1.

Akizungumza Dar es Salaam jana Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema maandalizi ya mechi hiyo yako vizuri na matumaini makubwa ya kutoka kifua mbele.Kamwaga alisema wachezaji wote wako vizuri na wana ari ya kuidungua 3Pillars, ili kujiwekea mazingira mazuri katika kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara.
3Pillars ambayo ni mechi yake ya tatu, awali ilifungwa bao 1-0 na Yanga katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa na baadaye kutoka sare na Coastal Union ya Tanga.Kamwaga amewataka wanachama na mashabiki wa Simba kufika kwa wingi uwanjani, ili kujionea watakavyo isambaratisha 3Pillars.
"Tunawaomba wanachama na mashabiki wetu wafike uwanjani kushuhudia timu yao kwani si siku ya kukosa kuliona pambano hilo ambalo litakuwa na burudani nzuri," alisema Kamwaga.Alisema viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 20,000 VIP A, sh. 10,000 VIP B na VIP C wakati viti vya njano na kijani ni sh. 5,000  

No comments:

Post a Comment