02 August 2013

TANESCO KUTATUA KERO ZA UMEME



Na Fatuma Mshamu
SHIRIKA l a Umeme n c h i n i (TANESCO) limeanza uboreshaji wa miundombinu yake ili kuondokana na tatizo la ukatikaji wa umeme mara kwa mara.Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Ofisa Mawasiliano na Mahusiano wa shirika hilo, Badra Masoud alipokuwa akibainisha maeneo yenye changamoto ya kukatika umeme na juhudi zinazofanywa ili kuondokana na tatizo hilo.

Alisema, pamoja na ukarabati unaofanywa katika miundombinu hiyo yapo maeneo ambayo umeme umekuwa ukikatika mara kwa mara."Ukiangalia kwa makini utagundua miundombinu hiyo ni ile iliyojengwa miaka mingi na tumewekeza nguvu kubwa zaidi kuiimarisha.
"TANESCO tumeimarisha miradi ya umeme katika uzalishaji, usambazaji na usafirishaji. Mradi wa uzalishaji wa Mwanza (Nyakato Plant) utazalisha megawati 60, Kinyerezi utazalisha zaidi ya megawati 900, Singida (upepo) 100, Kilwa energy 320 na mradi wa Symbion utazalisha megawati 600", alisema Badra.
Alisema, katika mradi wa City Center unaotekelezwa kati ya Serikali kupitia TANESCO na Serikali ya Finland wenye thamani ya euro milioni 25 utahusisha ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kilowati 132 chini ya ardhi.
Alisema, TANESCO kwa kushirikiana na ufadhili wa serikali ya Sweden chini ya Shirika lake la SIDA wataanza utekelezaji wa mradi kutoka Makambako mpaka Songea na mkandarasi ataanza kazi kabla ya mwishoni mwa mwaka huu.
Al i o n g e z a k uwa , c h a n g amo t o inayowakabili kwa sasa ni upungufu wa vifaa kwani wateja ni wengi, kwa mwaka huu pekee waliojiandikisha na kulipia ili waunganishiwe umeme ni 112,000 kati ya 150,000 wanaotakiwa kuandikishwa kwa mwaka.

.

No comments:

Post a Comment