27 August 2013

TAKUKURU YAWABURUTA KORTINI VIGOGO USHIRIKA



 Na Hamisi Nasiri, Nachingwea
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Nachingwea Mkoa wa Lindi imewafikisha mahakamani viongozi wawili wa chama cha msingi cha ushirika cha Naipanga wilayani humo kwa makosa ya kula njama ya kutenda kosa la rushwa,matumizi mabaya ya nyaraka na ubadhirifu wa fedha za chama hicho.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wi l aya , Co sma s Heme l e, Mwendesha mashtaka wa taasisi hiyo hiyo, Dismas Muganyizi aliwataja viongozi hao kuwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Salumu Tewa na mwandishi wa chama hicho, Mustafa Kanteu.
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja kwa kukusudia wanatuhumiwa mnamo Juni 30 mwaka huu kwa kutumia risiti yenye namba 027859 walijipatia kiasi cha shilingi 491,000 fedha za chama cha msingi cha Naipanga.
Muganyizi alieleza mahakamani hapo kuwa viongoz i hao walijipatia kiasi hicho cha fedha kwa madai ya kununulia kioo cha gari la mizigo ya chama hicho jambo ambalo lilibainika kuwa halikuwa la kweli ambapo kwa mujibu wa vifungu 22,28,32(1) namba 11 ya mwaka 2007 vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ni kosa. Mtuhumiwa Salumu Tewa yupo nje kwa dhamana huku Mustafa Kanteu akirudishwa rumande baada ya kukosa udhamini hadi Agosti 29 kesi hiyo itakapotajwa tena.

No comments:

Post a Comment