WANAR IADHA F a u s t i n e Mussa na
Msenduki Mohamedi, wanaoiwakilisha Tanzania katika michuano ya riadha ya Dunia
wanatarajia kuondoka leo Moscow, Urusi.Michuano hiyo ya
riadha ilianza tangu Agosti 10, mwaka huu nchini Urusi kwa kushiriki nchi
mbalimbali wakichelewa kuungana na wenzao.
Akizungumzia
kuchelewa kuondoka nchini kwa washiriki hao, Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha
Tanzania (RT), Suleiman Nyambui alisema wameamua kuondoka leo ili kutoa fursa
wanariadha hao kujiandaa vyema nchini."Tumeamua
wawakilishi wetu waondoke kesho (leo) kwa sababu ya kuwapa nafasi ya kujiandaa
zaidi, kama unavyojua zile nchi za ugenini tungewapeleka mapema wangejisahau
kwa kula vyakula vizuri na kulegea kimazoezi," alisema Nyambui.
Nyambui alisema
hawakuona sababu ya msingi kuwapeleka washiriki hao mapema Urusi kwa kuwa wao
wamepangiwa kukimbia mbio za Marathon Agosti 17, mwaka huu.Michuano hiyo inaendelea jijini Moscow, Urusi huku
ikishuhudia Mkenya Edna Kiplagat akijipatia medali ya dhahabu na kupaisha vyema
bendera ya nchi hiyo jirani
No comments:
Post a Comment