Na Leah
Daudi
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetengua
uamuzi uliotolewa na Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera kuwavua udiwani madiwani
nane wa chama hicho uliofikiwa juzi mkoani humo hadi itakapoamuliwa vinginevyo
na Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa itakayokutana
.Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Itikadi na Uenezi ya CCM, Nape Nnauye, alisema madiwani hao waliokuwa
wamesimamishwa kazi wanatakiwa kuendelea na shughuli zao kama kawaida
wakisubiri uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa
kitakachofanyika Agosti 23, mwaka huu, mkoani Dodoma.
Alisema kikao
hicho pamoja na mambo mengine kitapitia uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya CCM
mkoani Kagera.Nape alisema
utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye vyombo vya dola hasa
wabunge na madiwani uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Mkoa sio wa mwisho.
Alifafanua kuwa
uamuzi unatakiwa kupata baraka za Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na
ndio utekelezwe. Alisisitiza kuwa uamuzi ulitakiwa kupitia katika Baraza la
Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa ndipo uchukuliwe na sio vinginevyo.
Alisema tayari
wamepokea barua za kukata rufaa kutoka kwa madiwani hao za kukata rufaa kupinga
uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa kwa hoja kwamba taratibu zilikiukwa
wakati wa kufikia uamuzi huo.
Juzi
Halmashauri Kuu ya CCM ilitangaza kuwafukuza uanachama madiwani hao Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Bukoba ambaye pia ni Diwani wa Kashai, Yusuph Ngaiza,
Alexander Ngalinda (Buhembe), Samuel Ruhangisa (Kitendaguro), Dauda Kalumuna
(Ijuganyondo), Deus Mutakyahwa (Nyanga) na Robert Katunzi (Hamugembe).Wengine Richard Gasper (Mihembeni)
Mulundi Baduru Kichwabuta (Viti maalum).
No comments:
Post a Comment