- MAJINA YAO KUSAMBAZWA BALOZI ZOTE NJE
- SERIKALI YATANGAZA MSIMAMO WAKE
Na Waandishi Wetu
MAWAZIRI, wabunge, maaskofu, mapadri, wachungaji wanaohusika uagizaji na
uuzaji dawa za kulevya wametakiwa kutubu, kujisalimisha kwa Rais Jakaya
Kikwete, ndani ya wiki hii vinginevyo majina yao kusambazwa katika balozi zote duniani.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mchungaji wa Kanisa la
Kiinjili la Kipentekoste, William Mwamalanga, kutokana na wanafunzi wawili Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) na St.Gasper cha Morogoro kusalimisha kilo tano za heroine katika
kongamano la kidini lililofanyika TAG Mbeya.
Mbali na kujisalimisha vijana hao walitaja mawaziri
wawili, Naibu waziri mmoja, wachungaji, baadhi ya wabunge watatu wa viti maalum
na wabunge wastaafu wanaomiliki biashara kubwa ndani na nje ya nchi.
Mchungaji Mwamalanga alisema wamesikitishwa na
viongozi hao wakuu wa nchi ambao ndio wanatakiwa kuonesha mfano kwa Watanzania
kupiga vita dawa za kulevya, lakini wao ndio vinara wakuu wa kuwatumia vijana
hao kununua na kuyauza kinachoshangaza
zaidi ni watumishi wa dini,
maaskofu, wachungaji nao kuhusika na biashara hii kwa kutumia jina la Mungu kwa
namna tofauti na sote tunaonekana tunafanya hivyo,"alisema.
Mchungaji
Mwamalanga alisema wiki hii ni ya viongozi hao wa dini na serikali kutubu kwa
ukamilifu mbele za Mungu na ikiwezekana waache kazi hizo, kwani hawaitakii mema
nchi na Taifa lote kwa ujumla."Hii wiki
ya kutubu kwa mawaziri na wabunge waliotajwa pamoja na kutubu wajisalimishe
wenyewe kwa Rais Jakaya Kikwete wamweleze kwamba wao ni mabingwa wa kuuza dawa
za kulevya.
"Kama
hawatafanya hivyo wiki ijayo tutaanika majina yao
yote katika balozi mbalimbali duniani kwamba hawa ndio vinara wa dawa za
kulevya Tanzania,
hivyo wakifika katika nchi hizo wasiruhusiwe kufanya chochote wakamatwe,"
alisema.
Mchungaji
Mwamalanga alisema kuwa kusudi la kuanika majina yao
ni ili dunia iwatambue na kusisitiza kwamba wasipofanya hivyo wiki ijayo
watasambaza majina yao
duniani kote.
Alisema kuwa viongozi
hao wa dini wanatakiwa kujitambua na ndipo waweze kutubu ili waweze kupokea
nguvu ya Mungu kwa kutubu mbele zake.
Mc h u n g a j
i Mwama l a n g a a m e w a o m b a m a a s k o f u , wachungaji, mapadri,
mashekhe kuungana pamoja kuwafichua wenzao wanaohusishwa na tuhuma hizo kwa
kuwa wanajulikana.
Naye Mchungaji
wa Kanisa la Moroviani Iringa Abeid Mbisa alisema aliwashutumu viongozi hao wa
dini kwa kutumia jina la Yesu vibaya na kwamba watumishi wote wa dini
wanahusishwa na kashfa hiyo wakati hawahusiki.
"Wanatumia
jina la Yesu vibaya ninawashauri wapumzike kufanya kazi ya Mungu na badala yake
wafanye kazi nyingine na ikiwezekana watubu na kumtumikia
inavyopaswa,"alisema.
Alisema vijana
wamekuwa wakiharibiwa na watu ambao hawakuwategemea na badala yake wanapaka
matope makanisa na Taifa zima kwa ujumla.
Naye Mchungaji
wa Kanisa la TAG, Calvary Tempo, Daud Mwalonde alisema kitendo cha viongozi hao
wa dini, pamoja na viongozi wa serikali kuhusishwa katika sakata hilo la dawa
za kulevya kunadhoofisha nguvu ya Taifa.
Alisema vijana wanalala barabarani, wanakuwa na sauti ambazo sio zao na
nguvu ya Taifa imekwisha
kutokana na wengi kupoteza nguvu ya kufanya kazi kutokana na kutumiwa vibaya. "Ombi
langu kama mtu ameamua kuwa mtumishi afanye kazi ya Mungu asifanye Taifa
kuelekea pasipotakiwa na kama mtu ni mchungaji na kisha anashiriki kazi hizi
aachane na huduma hiyo kwa sababu haitakii mema Tanzania," alisema.
Wakati
huo huo, Tume ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, imesema
ina majina ya vigogo ambao wanahusika na uuzaji na usambazaji wa dawa hizo
ambapo wanachunguza kwa kina na pindi upelelezi ukikamilika watafikishwa
mahakamani.Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa kukabidhi msaada wa fedha wa
kiasi cha sh.milioni 2.5 kwa taasisi zisizo za kiserikali za Tandika Youth
Handcraft Group (TAYOHAG) Kwaya ya Nazareti, Kamishna wa tume hiyo, Christopher
Shekiondo, alisema kazi ya kupambana na dawa za kulevya inafanyika vizuri na
kwamba hadi sasa wana majina ya vigogo wanaojihusisha na dawa hizo, lakini
wanaendelea na upelelezi.
Alisema baadhi ya vigogo hao wengine
watafikishwa mahakamani wengine wamekimbia nchi na wengine bado hawajakamatwa
na wanaendelea kuw atu miavijana kufuata dawa hizonjeya nc hi.
“Tuna majina ya vigogo ambao
wanajihusisha na mtandao wa dawa za kulevya, lakini hatuwezi kuwataja kwa
majina kwa sababu lazima kwanza tufanye upelelezi wetu wa kina ili tuwakamate
na kama wamefikishwa mahakamani hatuwezi kuwataja hadi kesi iishe na wananchi
wengi wanataka kujua majina hayo ya vigogo,” alisema.
Alisema watu wanaokamatwa na dawa hizo
ni wale wanaotumwa na vigogo hao na ndiyo wanaokumbana na mkono wa sheria kwani
wabebaji wote ndio wanaokamatwa mara nyingi.Hata hivyo imekuwa vigumu kunasa
wahusika wakuu ambao ndio wanaowatuma wasafirishaji hao. Alisema si kila
Mtanzania anayekamatwa nje ya nchi akiwa na dawa za kulevya hutokea Tanzania, bali kutokana na wahusika kuwa na
mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi, wanachokifanya hutuma pesa ambapo mtu
anaweza kutokea nchi nyingine akaenda Brazil
na kisha kuchukua dawa hizo na kuziingiza nchini China.
Alisema hata hao wanaoingiza dawa hizo
nchini wanapita viwanja mbalimbali vya ndege vya kimataifa hadi kufikia hatua
ya kukamatwa. Alisema mwaka 2010 kumekuwepo na ongezeko kubwa la ukamataji wa
dawa hizo za kulevya nchini wakiwemo vigogo kutoka nje ya nchi. “Kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2012
kumekuwa na ongezeko kubwa la ukamataji wa dawa hizo ambapo kiasi cha dawa hizo
aina ya heroin kilikamatwa kilo zaidi ya 760 huku cocaine zilizokamatwa zikiwa
zaidi ya kilo 340 huku takwimu zikonesha kuwa mwaka huu kila wiki dawa hizo
hukamatwa,” alisema Shekiondo.
Pamoja na juhudi hizo lakini kuna
vyombo vingi vinavyohusika na udhibiti wa dawa hizo hivyo lazima kila sehemu
inayohusika na kazi hiyo iangaliwe ili kudhibiti zaidi.Alisema Watanzania 110 wamekamatwa
nchini Brazil ambapo
walikwenda kuchukua dawa hizo na wengine 35 wamekamatwa nchini China.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Tanzania
Labour Party (TLP), Augustino Mrema, ameitaka Serikali kuwakamata vigogo wote
waliotajwa katika kashfa hiyo.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mrema
alisema Tanzania inaiga sera
za watu wa Marekani, h i v y o i k umb u kwe k uwa Marekani ilimkamata Jenerali
Manuel Noriega aliyekuwa Rais wa Panama kwa kuunga mkono matumizi ya
dawa za kulevya nchini mwake."Hivyo ni jukumu la Serikali,
kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kuruhusu sheria kuchukuwa mkondo wake
kwa wahusika wote kwani ni aibu kwa Taifa,"alisema Mrema.
Akifafanua zaidi alisema kama Serikali
haijachukua hatua za haraka ikumbuke kuwa kashfa hiyo ndio iliyosababisha
kupinduliwa kwa Serikali ya nchi ya Panama na kuongeza hata mataifa
mengine yatatuchukia kwa kuendelea kukaa kimya.Alisema hata kama taarifa hizo hazina
ukweli wa asilimia 100, lakini zina ukweli wa asilimia 80 na kuongeza kuwa kama wanataka ushahidi wa asilimia 100 basi wasubiri
mpaka atakaporudi Yesu au Mtume Muhammad ili awathibitishie.
Alisema hali imekuwa mbaya sana katika nchi yetu,
watu walionekana wakisafirisha Twiga kupitia uwanja wetu wa ndege na sasa
wameamua kusafirisha dawa za kulevya, kupitia nchini.Mrema amevitaka vyombo vya habari
kutaja hadharani majina ya watu wote wanaojihusisha na mtandao huo ili kutoa
fundisho kwa wahusika wengine.
"Imefika wakati lazima tuwe
majasiri kwa kuwataja majina hadharani, potelea mbali tutawaomba samahani
baadae maana sasa hali inatisha,"alisema Mrema.Alisema ikiwa mawaziri na wabunge wanatajwa kuhusika na dawa
za kulevya, halafu wenyewe wanakataa wakidai wanasingiziwa ni lini watakubali
ukweli kila siku wanasingiziwa wao tu.
inasikitisha sana kwamba watenda maovu kama hayo badala ya kutajwa ili tuwafahamu,tuwaepuke na kupelekwa mahakamani majina yao tena yatapelekwa kwa rais!!!!! kufanya nini ili hali rais anayo yake na hajachukua hatua yoyote. wewe mwamalanga kwa unalotaka kufanya hakuna utakalokuwa umelisaidia taifa hili
ReplyDeleteJE NI KWELI RAIS WETU ANAYO NIA YA DHAATI YA KUPAMBANA NA TATIZO HILI NA MENGINEYO MENGI?SINA IMANI NA RAIS HATA CHEMBE.NCHI IKO KWENYE MATATIZO MAKUBWA SANA.
ReplyDeleteswala la kupambana na tatizo la madawa ya kulevya ni la wote rais ni sehemu ya wananchi isipokuwa huyu mchungaji ni moga wa kutaja -mbona anaonekana kusemasema sana kwanza ana uhakika au anafata anayoambiwa na hao wasomi.wasomi gani wa chuo kikuu wanakubali kutumiwa kiasi hicho.weka wazi majina ila ujuwe kujitetea maana utakuwa umechafua watu kwa zege kali kuwasafisha utaweza?
Deletekama huyu mchungaji ana nia ya dhati na anaipenda nchi yake ni vyema awataje hao watu otherwise itaonekana anatafuta umaarufu kwa kutumia majina ya watu.
DeleteHuo utaratibu unaosemwa wa kujisalimisha kwa Rais mimi siuoni kuwa ni mzuri.Sijui kama kweli hao watu na hizi taarifa ni za kweli,na huo utamaduni wa waovu(wenye dhambi kwa mujibu wa mchungaji huyo)kuwaelekeza kwa Mkuu wa nchi.Wajibu wa mchungaji/padri ni kutubisha roho na kaisari kazi ni kuadhibu mwili.Kwa hiyo mch apeleke majina kwa kaisari asihusike mambo ya sheria.mwili utaadhibiwa na roho itaenda mbinguni kwa sababu imetubu.
ReplyDeletekweli kabisa. rais naye anaweza kuwa muhusika
DeleteNasikitika sana kwani hao ambao tunadhani tumewapa nchi kwa kutuongoza hao hao ndio ambao wanatuua jamani. sasa tufanyeje. Mkuu wa nchi , sasa gurudumu linakuangukia wewew. tumia rungu jitoe muhanga kwani ndio kazi yako ya kuokoa na kutetea nchi hii
ReplyDeleteNingekuwa mimi mwenye runge ningepa mchana peupe kwa ambao watuulia taifa letu
ReplyDeleteHivi sisi watz tuna laana gani? hata viongozi wa dini wana woga wa kukemea wadhambi mpaka rais atoe ruhusa hii imekaaje?. Aibu kwao wanatupoteza muda......
ReplyDeleteNI VEMA WOTE WALIOTAJWA WAJIUZULU ILI UCHUNGUZI UFANYIKE KWA UHURU NA UWAZI
ReplyDeletewahusika ni wale wenye madaraka, wakitajwa nchi itayumba hivyo jukumu ni letu wananchi
ReplyDeletenchi hii siyo kama wengi mnavyodhani. Mfanyabiashara ya madawa ya kulevya siyo kama muuza cd feki. rais yeyote wa nchi duniani, ndiye amiri jeshi mkuu na wala hapaswi kubezwa kama wengi mnavyosema. matatizo ya Tanzania yalikuwepo toka enzi za ukoloni, hata hivyo usidhani hata aje rais yupi matatizo yako yataisha kwa kumchagua yeyote awe rais, kwanza fanya kazi na ujitume. hili ndilo litakalokuondolea matatizo. vijana wa tanzania tuache kulalamika hata mambo ambayo sisi hatuna uwezo nayo. Mchungaji yupo sahihi kwani ametoa mda wa hao kutubu na kama hawatafanya hivyo sheria itachukua mkondo wake. Kilo tano siyo mchezo.
ReplyDeletehiyo ni kweli,ni serikali na taasisi ya Urais ilaumiwe maana hao ndo wanawalea ndugu zao na marafiki wao ambao wako kwenye system wengine ni matajiri tu wa kutupwa wana support chama tawala cha CCM,wengine wako serikalini ni wazito marafiki wa karibu waliomweka madarakani rais ambao anawajua na sio wasafi, wengi wao wamepewa ahsante nyingi ni vigumu tena kwa mkuu wa nchi kuwasaliti,pengine hizo hizo pesa chafu ziliyumika kwenye kampeni,watu hawa hawaguswi na chombo chochote cha usalama wa nchi hii.
ReplyDeleteTumechoka kusikia neno "Vigogo" wakati majina yao kamili hayatajwi. Huu ni usanii tu, hakuna umakini katika jambo hili kwa sababu wasemao ndiyo wahusika.
ReplyDelete