15 August 2013

POLISI YAKAMATA GUNIA 352 ZA BANGI Na Mwandishi wetu, Arusha
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia wakazi watano wa kijiji cha Kisimilijuu wilayani Ar ume r u , wa k i t u h umiwa kukamatwa na magunia 352 dawa za kulevya aina ya bangi.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema magunia hayo yalikamatwa jana, kutokana na msako maalumu unaoendelea mkoani humo.

"Tumeyakamata wakati wa operesheni ambayo tumeiendesha kwa siku mbili katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha na kufanikiwa kupata magunia hayo ambapo 225 tayari yametekezwa kwa moto na yaliyobaki yatachukuliwa kama uthibitisho mahakamani,"alisema Kamanda huyo.
Aliwataja watuhumiwa watano waliokamatwa wakati wa msako huo kuwa ni Esubhati Daudi (24), Atumii Daudi (28), Lemali Saitoti (40), Thomas Semile (60), Lomayani Thomas (42), wakazi wa kijijini hapo walikamatwa.
Alisema watuhumiwa wote hao watafikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya upelelezi kukamilika. Alitoa onyo kuwa jeshi hilo halitawaonea haya watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo, kwa kuwa wanaenda kinyume cha sheria ya nchi.

No comments:

Post a Comment