LONDON, Uingereza
WATAALAMU wa lishe na maabara wamegundua njia mbadala ya kuzalisha
nyama bandia maarufu kama 'burgers' kwa kutumia tishu zinazotoka katika seli za
ng'ombe.Kwa mujibu wa
utafiti uliofanywa kwa siku kadhaa na kuripotiwa jana na Shirika la Habari la
AP ulibainisha kuwa, ingawa utafiti huo uliwagharimu wataalamu zaidi ya Euro
300,000 kuzalisha, wameweza kufikia hatua nzuri
."Lakini hii
si burger kama hizi za kawaida inaonesha ni nzuri na watu walijaribu kuionja
mjini London, siku ya Jumatatu. Nyama hii iliweza kuzalishwa kupitia maabara
kutokana na seli za ng'ombe," ilieleza sehemu ya utafiti huo.
Kwa mujibu wa Mark Post ambaye alikuwa
miongoni mwa wataalamu waliongoza timu hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Maastricht
kilichopo Netherlands ambaye alifanya utafiti huo kwa zaidi ya miaka mitano
alisema hayo ni matumaini.
"Ninaamini kuwa kutengeneza nyama
kupitia maabara itasaidia kwa hatua kubwa kutatua tatizo la chakula na
kupunguza tatizo la uharibifu wa mazingira," alieleza Post katika utafiti
huo.
Mbali na hayo, Post alisema kuwa
mafanikio hayo hayawezi kuzuia utafiti kuendelea.
"Ili burger hii iweze kufanikiwa
katika viwango bora ni lazima ichunguzwe na ikiwezekana kuionja kama kitu cha
kawaida," alisema.
Hata hivyo, kwa mujibu wa utafiti huo
nyama yao ilitengenezwa kutokana na seli za misuli ya ng'ombe ambayo
ilichukuliwa na kuyeyushwa na hatua ya mwisho ikachanganywa na vitu vingine.
"Pia tuliweza kuchanganya chumvi,
egg powder, breadcrumbs, red beet juice and saffron," iliongeza utafiti
huo.
Aidha, Post na watafiti wenzake kwa
mujibu wa utafiti huo walichukua seli za ng'ombe na kuzichanganya katika
mpangilio wa lishe ambao uliwasaidia kufikia hatua hiyo ya kutengeneza nyama
bandia.
"Muonekano wa ukusanyaji wa seli hizo ulipangiliwa katika chembe ndogo
ndogo zaidi ya 20,000 ili kutengeneza gramu 140 za nyama ya burgers,"
aliongeza Mtafiti
No comments:
Post a Comment