27 August 2013

NSSF KUKUSANYA BILIONI 706/- KUTOKA KWA WANACHAMANa Fatuma Mshamu
SHIRIKA la Hifadhi ya Taifa (NSSF) linatarajia kukusanya kiasi cha sh. bilioni 706.41 kutoka kwenye michango ya wanachama wake katika mwaka huu wa fedha.Meneja kiongozi wa huduma kwa wateja Eunice Chiume alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kinatokana na uandikishaji wa wanachama 169,241 wa mpango wa lazima na wanachama 85,158 wanaojiunga kwa hiari.

Alisema katika kipindi h i k i wa a j i r iwa 3 , 0 6 2 wanatarajiwa kuandikishwa na kuunganishwa na waajiri 19,231 wa sasa na kufanya ongezeko la asilimia 84.07.Chiume alisema, "Kiasi cha sh. bilioni 199 kitalipwa kwa wanachama watakaoacha kazi au kustaafu huku kiasi cha sh. bilioni 5.19 kitalipwa kwa ajili ya mafao ya matibabu kwa wanachama 254,399."
Alisema, katika mwaka huu wa fedha shirika linatarajia kuwekeza sh. bilioni 951.4 ukilinganisha na sh.bilioni 751.4 ambazo ziliwekezwa katika mwaka wa fedha 2012/13 sawa na ongezeko la asilimia 21.06.
Alisema kuwa shirika linatarajia kukusanya mapato ya sh. bilioni 181.1 kutoka kwenye vitega uchumi ukilinganisha na mapato ya sh. bilioni 120.1 zilizokusanywa mwaka jana, pia thamani ya mfuko kwa mwaka jana ilikuwa sh. trilioni 2.1 na inatarajiwa kuongezeka na kufikia sh. trilioni 2.6 sawa na ongezeko la asilimia 19.23.Aidha aliongeza kuwa katika mashindano mbalimbali ya michezo iliyofanyika mwaka huu timu ya mpira wa pete ya Business Times Limited iliibuka na ushindi

No comments:

Post a Comment