02 August 2013

UCHACHE HAATI ZA MAJENGO KIKWAZO CHA MAENDELEO Na Grace Ndossa

KUKOSEKANA kwa umiliki wa rasilimali ardhi na majengo (Land Title Deeds) miongoni mwa Watanzania kunarudisha nyuma upatikanaji wa maendeleo hapa nchini.Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha kamati cha taasisi hiyo kilichokuwa kikijadili umuhimu wa kuwa na hati ya umiliki wa rasilimali hiyo kuwa ni asilimia tatu tu ya Watanzania mpaka sasa ndiyo wenye hati za umiliki huo
. "Tunashindwa kupata maendeleo kutokana na kwamba hatuna hati hizi ambazo zinatumika kuombea mikopo katika taasisi za fedha," alisema Simbeye na kuongeza kuwa rasilimali isiyohamishika ndiyo inayokubalika zaidi katika kupata mikopo.
A l i s e m a k i k a o walichofanya kilikuwa ni mwendelezo wa vikao vinavyoendelea kufanyika kwa ajili ya kuungana na vile vinavyofanywa na sekta ya umma katika mbinu za kutaka kurahisisha upatikanaji na kutaka kuboresha mazingira ya biashara.

Alisema pia viwango vya Benki ya Dunia (WB) vinaonesha Tanzania ipo nyuma sana, hivyo kuna kila sababu ya kuhakikisha maboresho yanafanyika haraka ili kila mtu aweze kuwa na hati ya umiliki wa ardhi na majengo bila usumbufu.

Alisema mchakato wa rasilimali hizo kutakiwa kuwa na hati za umiliki ulianzishwa mwaka 2009 na ilipofika mwaka 2010 Serikali ilikubali lakini utekelezaji wake umekuwa wa kiwango cha chini sana.

"Kwa s a s a k ama t i yetu inajadili viwango vilivyowekwa na Benki ya Dunia na taarifa ya Serikali ya utekelezaji wa mpango kazi wa maboresho ya mazingira ya biashara na uwekezaji (ROADMAP) katika kipindi cha robo mwaka ya tatu na nne ya mwaka wa fedha 2012/13," alisema.

Alisema pia kamati hiyo imejichimbia kujadili kwa kina vikwazo mbalimbali vilivyopo katika utekelezaji wa makubaliano hayo ili kuja na mapendekezo ya kuisukuma Serikali kuharakisha suala hilo kwa masilahi ya taifa na watu wake.

Al i s ema Mi l l e n i u m Challenge Corporation kutoka Marekani imetenga dola milioni 800 za Marekani ambapo sehemu ya fedha hizo zitatumika katika masuala ya ardhi ikiwemo kupima na kutoa hati za umiliki.

Mshauri wa masuala ya wajasiriamali TPSF, Dkt. Donath Olomi alisema nchi ikifikia viwango vya kimataifa vya utoaji wa hati za umiliki ardhi na majengo na vibari mbalimbali umaskini utapungua kwa asilimia kubwa.

No comments:

Post a Comment