02 August 2013

MAITI YAOKOTWA MBEZIMWANAUME mmoja ambaye hakufahamika jina amekutwa amekufa majira ya saa 10:00 alfajiri huku mwili wake ukiwa umeharibika vibaya huko Mbezi Luguruni Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam anaripoti, Frank Monyo. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.
Camilius Wambura alisema marehemu anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 25-30 alikutwa amelala kifudi fudi huku mwili wake ukiwa umeharibika vibaya kiasi kwamba sura yake haikuweza kutambulika. Kamanda huyo alisema, marehemu alikutwa amevaa suruali yenye rangi ya kijivu huku fulana yake ikiwa pembeni yake, hivyo kutokana na maiti yake kuharibika ambapo daktari kutoka Hospitali ya Mwananyamala alifika na kuufanyia uchunguzi mwili huo na kuzikwa maeneo hayo ya Mbezi Lug

No comments:

Post a Comment