Goodluck
Hongo na Hytham Mushi
SIKU mbili tangu
kuanza kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mbunge wa Iramba Magharibi,
Mwigulu Nchemba, ameanza kuwasha 'moto' bungeni kwa kuhoji sababu za Mwenyekiti
wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Katibu wake, Dkt. Willbrod Slaa, kuendelea kuwa
huru, wakati wanastahili kuwa jela kwa kusababisha mauaji ya raia.
Nchemba
alitoa kauli hiyo mjini Dodoma jana wakati akiuliza swali la nyongeza. Katika
swali hili mbunge huyo alihoji ni kwa nini Serikali imeshindwa kuwachukulia
hatua viongzi wa vyama vya siasa wanaosababisha vurugu na mauaji ya raia.
"Ni
lini Serikali itachukua hatua kwa viongozi wa vyama vya kisiasa wanaosababisha
maafa ikiwemo mauaji ya Ndago, Arusha, Morogoro na Iringa, kwani kama kweli
hatua zingechukuliwa basi Mbowe na Slaa sasa hivi wangekuwa tayari wako
jela," alisema Mwigulu.
Kauli
hiyo ilisababisha Bunge kuzizima kwa kelele kutokana na kutajwa kwa Mbowe na
Dkt.Slaa. Swali hilo lilijibiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala
Bora), George Mkuchika, ambapo alisema kuwa nchi hii inaongoza kwa kufuata
utawala bora.
"Katika
hili kuna mihimili mitatu ya Bunge,Mahakama na Serikali Kuu, hivyo kwa hali
hiyo kuna kesi ambazo zipo mahakamani, hivyo wanaiachia mahakama katika suala
hilo," alisema Mkuchika.
Baada
ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu ndipo baadhi ya wabunge
walipoomba miongozo juu ya kauli mbalimbali zilizotolewa bungeni juzi na jana.
Mbunge
wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA) aliomba mwongozo kwa Naibu Spika, Job
Ndugai, akitumia kanuni ya 68 (7) ibara ya 61 na 64 kuwa inakataza kwa mbunge
kutoa maneno ambayo yanamchafua mtu mwingine hivyo alimtaka Mwigulu Nchemba
afute kauli yake.
"Naomba
mwongozo wako kupitia ibara ya 68 (7) kanuni ya 61 na 64 ya Bunge inamzuia
mbunge kutoa maneno ya kumchafua mtu mwingine kwani kuna mauaji ya aliyekuwa
mwenyekiti wa CHADEMA wilayani Arumeru kuuawa kwa kuchinjwa na mashine ya
kukatia miti/magogo na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), licha ya
kukamatwa watu hao, lakini pia walitoroka wakiwa na pingu mikononi hadi leo
hawajulikani walipo; hivyo kwa suala hilo naomba Mwigulu Nchemba afute kauli
yake," alisema Wenje.
Kufuatia hali hiyo
Naibu Spika Bw.Job Ndugai alisema atalitolea ufafanuzi yeye mwenyewe baadaye
kidogo.
Mie nadhani mwigulu ni mbwia unga- muonekano wake, mwenendo wake na hata apimwapo mental scan anaonekana ameathirika sana na vitu fulani. May be huenda tatizo likawa linasababishwa na jinsi alivyowhi kuugua mwaka 2003 - 2007
ReplyDeleteMwigulu Mchemba is good for nothing MP.
ReplyDeleteNchemba anaficha makosa kwa kuwakosoa wasio na makosa . C CM inashindwa kupata viongozi wenye busara. Ni aibu kuongozwa kitaifa na mtu asoye na uwezo.
ReplyDeleteKuna masuala muhimu zaidi kushughulikiwa kama migogoro na nchi jirani nilitegemea kumuona mwigulu mstari wa mbele kumshauri rais namna ya kupambana lakini mind set ya wanaccm wengi wameiweka kupambana na chadema kwa kuwa ni mafisadi hawako tayari kupoteza dola
ReplyDeleteHuyu jammaa anataka uwaziri amesahau ccm imebakiza mwaka mmoja tuizike na yeye akiwa ndani
ReplyDelete