Anneth
Kagenda na Salma Mzee
TARATIBU za kuanza
kuwakabidhi barua za kuwaachisha kazi wafanyakazi wa Idara ya Karakana na
Ujenzi katika Shirika la Reli Tanzania
na Zambia
(TAZARA), uliokuwa uanze jana, umekwama kwa sababu ambazo hazikujulikana mara
moja
.B a r u a z a wa f a
n y a k a z i walioachishwa kazi zilikuwa zianze kukabidhiwa jana mchana,
lakini muda huo ulipofika ilitolewa taarifa kuwa utaratibu huo umeahirishwa kwa
kile kilichoelezwa kuwa mhusika alipigiwa simu ili asitishe hatua.
Hali hiyo ilijitokeza
makao makuu ya TAZARA, Dar es Salaam jana, hatua iliyosababisha wafanyakazi hao
kuanza kuimba nyimbo za kejeli zenye ujumbe kuwa menejimenti inawaogopa kuwapa
barua za kuwaachisha kazi.
Uamuzi wa kuwaachisha
wafanyakazi 1,067 ulifikiwa juzi ukihusisha wafanyakazi mbalimbali kutoka
vitengo sita katika shirika hilo, lakini waliotangazwa kwenye awamu ya kwanza
ya kukabidhiwa barua walikuwa wafanyakazi wa vitengo vya karakana na ujenzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania ( T R AW U ) , Ya s
i n M l e k e , aliwaambia waandishi wa habari kuwa wafanyakazi wa vitengo
vinne, kati ya sita walikuwa hawajatangaziwa uamuzi wa kupewa barua
No comments:
Post a Comment