19 August 2013

MSHINDI WA NYUMBA AIRTEL,AKABIDHIWA FUNGUO




 Meneja wa Airtel mikoa ya Kusini, Bw. Beda Kinunda (kulia),akimkabidhi funguo mshindi wa
nyumba ya kwanza ya 'Airtel Yatosha'. Tukio hilo limefanyika jana kutoka Frelim Mjini Iringa,
Bw. Sylivanus Wanga, ambapo katikati ni mke wa mshindi huyo Bi. Veronica Wanga na Meneja
Uhusiano wa Airtel, Bw. Jackson Mmbando.

Na Mwandishi Wetu

MSHINDI wa wa nyumba ya kwanza ya Airtel Yatosha yenye thamani ya sh. milioni 65 iliyotolewa na Kampuni ya Airtel, mwishoni mwa wiki hii amekabidhiwa ufunguo wa nyumba yake.Makabidhiano ya funguo hiyo kwa mshindi, Silvanus Juma, yalifanyika mwishoni mwa wiki hii mkoani Iringa. Pia alikabidhiwa na cheti kinachoonesha kwamba yeye ni mshindi wa kwanza wa nyumba hiyo kati ya tatu zinazoshindaniwa kupitia promosheni ya Airtel Yatosha.


Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema makabidhiano ya funguo ni ya awali lakini Alhamisi ya wiki hii mshindi huyu, atakabidhiwa rasmi nyumba yake iliyopo maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Alisema Airtel inayo furaha kubwa kumkabidhi mshindi wao huyo zawadi hiyo na itaendelea kutoa zawadi zilizo bora kwa wateja wake nchi nzima kupitia promosheni mbalimbali zinazoendeshwa na Kampuni hiyo.

"Kama alivyo na furaha mshindi wetu ndivyo na sisi tunavyofurahi na hii sio kikomo bado kuna zawadi mbalimbali kwa wateja wa Airtel nchi nzima na cha muhimu ni wao kujiunga na vifurushi mbalimbali vinavyopatikana kwenye promosheni hii ya ya Airtel yatosha shinda nyumba 3 mbalimbali za Airtel ili kushinda," alisema Mmbando.

Hadi sasa Airtel imeweza kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja wake nchi nzima ambapo imetoa sh. milioni 37 kwa washindi 37 na inaendelea na promosheni hiyo ambayo itadumu kwa siku 90, sambamba na hilo nyumba mbili kati ya tatu zilizopo Kigamboni bado zinashindaniwa kupitia promosheni hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Juma alisema zawadi hiyo ya nyumba ni bahati ya kipekee ambayo hakuitarajia hapo awali na hata alipopigiwa simu hakuamini kwa sababu alijua kitu kama hicho hakiwezekani na hawezi kupata nyumba katika msimu kama huo.

"Nilipopigiwa kwanza nilijua ni utani, pengine mtu amejisikia tu kunitania lakini nilipigiwa tena na hapo ndipo nilipoanza kuamini," alisema.
Juma aliibuka mshindi wa nyumba hiyo baada ya kuchezeshwa kwa droo ya kwanza makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam mwisho mwa Julai.

No comments:

Post a Comment