Na Pamela Mollel, Simanjiro
SERIKALI kupitia Idara ya Madini, Kanda
ya Kaskazini imefungua migodi minne iliyopo kitalu D katika migodi ya madini ya
Tanzanite Mererani,wilayani Simanjiro mkoani Manyara iliyokuwa imefungwa baada
ya kutokea mauaji ya mchimbaji yaliyotokea hivi karibuni
.Mgodi huo
ulifungiwa kufanya kazi kwa takriban mwezi mmoja ili kupisha uchunguzi wa kina
kubaini chanzo cha mchimbaji wa madini aliyepoteza maisha hivi karibuni,
shughuli za uchunguzi zilikuwa zikiendeshwa na Jeshi la polisi wakishirikiana
na idara ya madini Kanda ya Kaskazini Mchimbaji William Mushi wa Kampuni ya
mwekezaji ya Tanzanite One inayochimba katika kitalu C alidaiwa kuuawa ndani ya
mgodi baada ya kundi la wachimbaji kuingia eneo hilo kinyemela.
Akithibitisha
kufunguliwa kwa mgodi huo Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Benjamin
Mchwampaka, alisema baada ya uchunguzi kukamilika waliamua kuufungua ili
wachimbaji waweze kuendelea na shughuli za uchimbaji.
"Tumefungua migodi hiyo ili kupisha shughuli za
uchimbaji kuendelea na pia tunasisitiza kila mgodi uchimbe eneo lake bila
kuingilia mwingine ili kuepusha migogoro ya kila siku," alisema,"
Mchwampaka
No comments:
Post a Comment