06 August 2013

MMALAWI ATAMBA KUMDUNDA FRANCIS CHEKA


Ester Maongezi
BONDIA nyota wa ngumi za kulipwa nchini Malawi, Chimwemwe Chiotcha amewasili nchini na kutamba kuwa atamtwanga bondia asiyekuwa na mpinzani nchini Tanzania, Francis ìSMGî Cheka katika pambano lao la uzito wa super-middle lililopangwa kufanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro.

Chimwemwe ambaye hajawahi kupoteza pambano nchini Malawi zaidi ya kupigwa kwa pointi na Cheka Desemba 27, mwaka jana alisema kuwa amekuja kulipiza kisasi huku akiponda matokeo ya awali kuwa Cheka alibebwa sana.
Alisema hajui ni ushindi wa aina gani atakaoupata kwa bondia huyo, kwani Knock Out (KO) au Technical Knock Out (TKO).
"Cheka amejiandaa sana, sikuridhika na matokeo ya awali na ndiyo maana nimeamua kuja kurudiana naye, najua nitaibuka na ushindi,î alisema Chimwemwe.
Alifafanua kuwa si kweli kuwa kila bondia aliyepigana na Cheka na kushindwa, sio kama hajui ngumi za kulipwa zaidi ya hofu tu kutoka kwa mabondia hao. Mimi nimedhamiria kufanya kweli na ninajua nitashinda, hii ni fursa yangu,î alisema Chimwemwe ambaye ni mwanajeshi wa Jeshi la Malawi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Best Man Promotion inayoaandaa pambano hilo, Zumo Makame alisema kuwa maandalizi ya pambano hilo yamekamilika na siku hiyo kutakuwa na mapambano makali na ya kusisimua.
Makame aliyataja mapambano hayo kuwa, Deo Njiku atawania ubingwa wa Taifa wa Shirikisho la Masumbwi Tanzania (PST), dhidi ya Cosmas Cheka, Rashid ìSnake Manî Matumla atazichapa na Maneno ìMtambo wa gongo ì Oswald na bondia mwingine kutoka Malawi, Bright Mdoka atazipiga na Jitu Samia.
Mapambano mwngine kwa mujibu wa Makame ni Nasibu Mkude atapigana na Juma Kihiyo katika uzito wa super welter bout, Juma Afande v Epson (featherweight) na Karim Mandonga dhidi ya Ramadhan Agogo katika uzito wa superwelter

No comments:

Post a Comment