Na
Daud Magesa, Mwanza
BODI ya Utalii Tanzania (TTB), Kanda ya Ziwa, imewataka
wafanyabiashara wa Jiji na Mkoa wa Mwanza, kuchangamkia fursa za uwekezaji wa
mahoteli makubwa yenye hadhi kukuza utalii.Rai hiyo ilitolewa jana na
mwakilishi wa TTB Kanda ya Ziwa,Gloria Munhambo, kwenye mdahalo wa wadau wa
Maendeleo ya Mkoa wa Mwanza, ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari
mkoani humo (MPC)
.Mdahalo huo ulilenga
kujadili changamoto mbalimbali na jinsi ya kutumia fursa zilizopo mkoani humo
kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.M u n h a m b o a l i s e m
a wafanyabiashara wengi wa jiji la Mwanza,bado hawajachangamkia fursa zilizopo
katika sekta ya utalii kwa ajili ya maendeleo, kukuza na kuvutia watalii.
Alisema ili kuvutia utalii, wanapaswa kuwekeza kwa
kujenga miundombinu ya mahoteli yenye hadhi na kuongeza vitanda kwa sababu
hoteli zizopo bado ni chache zisizokidhi mahitaji.
"Bodi ya Utalii tunasisitiza uwekezaji katika
sekta ya utalii.Tuna vivutio vingi,tatizo wafanyabiashara hawajawekeza kwenye
mahoteli na kuongeza vyumba vya kulala wageni," alisema Munhambo.
Alisema Serikali katika Sera ya Utalii ya mwaka 1991
inasisitiza ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia sekta ya utalii, lakini changamoto
kubwa ni uwekezaji mdogo katika sekta hiyo kutokana na jamii kushindwa
kuchangamkia eneo hilo.
Aidha, mwendeshaji wa mdahalo huo,Yasin Ali, alisema
pamoja na fursa za uwekezaji lakini wafanyabiashara wengi wa mkoani hapa,
wamelenga kupata faida tu.
"Bado tupo nyuma katika kutumia fursa zilizopo
kwenye sekta ya utalii. Juzi walikuja watalii wakihitaji kuzunguka mji wa
Mwanza kwa saa 8 halafu waendelee na safari yao,lakini gharama walizoambiwa
waliamua kuondoka," alisema Ali.
Hata hivyo, wadau wa mdahalo huo walitoa mwito kwa
Kituo cha
U w e k e z a j i T a n z a n i a (TIC),kubadili sera
zake ili kusaidia wawekezaji wa ndani badala ya wawekezaji wa kutoka nje ili
wanufaike na fursa zilizopo
No comments:
Post a Comment