Na Rachel Balama
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amewataka
wananchi wa Mlonganzila ambao hawajalipwa fidia baada ya nyumba zao kubomolewa
kupisha mradi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili(MUHA’s), kuruhusu
mradi huo uendelee na kuahidi kwamba watalipwa fidia zao ifikapo Septemba,
mwaka huu
.Pinda aliyasema hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa
akizungumza na wananchi hao alipotembelea eneo hilo la mradi.
Alisema anatambua kwamba katika eneo la
mradi kuna wananchi 91 ambao bado hawajalipwa fidia zao na kuwataka wananchi
hao kutokuwa na wasi wasi. Alisema wataanza kulipwa fidia hizo mwezi ujao.
Alisema fedha za fidia zimetengwa
kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2013-2014 ambapo ulipaji wa fidia umechelewa
kwa sababu ilikuwa ikisubiriwa bajeti ipitishwe.
“ K w a k u w a b a j e t i
imekwishapitishwa mambo yote yatakwenda kama yalivyopangwa, haikuwa dhamira
yetu fidia zenu zichelewe isipokuwa tulikuwa tunasubiri bajeti ambayo tayari
imepitishwa,” alisema Pinda.
Pinda alisema katika eneo hilo la mradi
zitaanza kujengwa huduma muhimu kama barabara, maji na umeme na baada ya hapo
yatafuata mambo mengine.
Katika eneo hilo la Mlonganzila lililopo Kibamba, Manispaa
ya Kinondoni tayari wananchi wapatao 2,335 walikwishalipwa fidia zao na kubakia
wananchi 91 ambapo wameahidiwa kulipwa fidia mapema mwezi ujao
No comments:
Post a Comment