Na S t e v e n Wi l l i am, Muheza
SERIKALI
mkoani Tanga imesema kuwa mgogoro wa shamba la mkonge la Kibaranga wilayani
Muheza na wananchi 1,128 wa Derema Tarafa ya Amani wilayani Muheza sasa
umefikia mwisho.Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Chiku Gallawa katika kikao cha wadau wa mkonge na viongozi kutoka kata ambazo
zina mgogoro wa shamba hilo
katika ukumbi wa Bomani wilayani Muheza
. Alis ema k uwa s as a mgogoro huo
ufikie mwisho kutokana na mvutano mkubwa na wa miaka mingi kati ya wananchi na
Serikali juu ya wananchi kupatiwa ardhi katika shamba la mkonge Kibaranga.Hatua hiyo ya mgogoro huo umekuja baada
ya Serikali kuchukua mashamba ya wananchi wa Derema kwa kuwalipa fidia kupisha msitu
wa hifadhi ya serikali na kuwaahidi watawapa eneo la kulima mashamba katika
shamba la mkonge Kibaranga toka mwaka 2012 mpaka leo hawajapewa.
Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu
alisema kuwa Rais Jakaya Kikwete alipokuja Tanga a l i z u n g umz i a k u h u
s u migogoro ya mashamba hayo na kuagiza sasa ifike tamati.Mbunge wa Jimbo la Muheza, Herbert
Mntangi alisema kuwa Rais Jakaya Kikwete anasubiri maamuzi ya kikao hicho
yakimfikia mezani kwake ataifuta hati ya shamba la Kibaranga ili wananchi wapewe
kwani haiwezekani kumpa mkulima hati kabla ya mwanzo haijafutwa wananchi wawe
watulivu.
Kwa u p a n d e wa k e Mkurugenzi Mkuu
wa Bodi ya Mkonge Tanzania Hamisi, Mapinda alisema kuwa tayari Serikali imetoa
sh. milioni 200 kwa ajili ya kuwapimia mashamba wananchi.Ofisa madeni kutoka CHC Robart Ngajilo
alisema kuwa mgogoro huo ufikie tamati ili wananchi wapewe mashamba katika
shamba la mkonge Kibaranga.
M k u r u g e n z i w a Halmashauri ya
Wilaya ya Muheza, Ibarahimu Matovu alifafanua katika taarifa kwa mkuu wa mkoa
jinsi ya wananchi hao kupewa mashamba katika shamba la mkonge Kibaranga
Kwa
u p a n d e wa k e Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Amiri
Kiroboto alimtaka mkuu wa mkoa kutoa ahadi kwamba wananchi watapata lini
mashamba ambapo mkuu wa mkoa alijibu kumambo hayo yanakwenda haraka sasa
wakulima wataanza kulima kipindi hiki cha vuli katika shamba hilo la mkonge
Kibaranga, mgogoro sasa basi.
No comments:
Post a Comment