Na Mwandishi Wetu
MAKAMU
wa Rais D k t . M o h a m e d Gharib Bilal ametoa rai ya kuongezwa kwa kasi ya
uwekezaji wa elimu na uwezo wa matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano
- Tehama kwa vijana nchini ili waweze k u i s h i kwe n y e e n z i waliyomo
inayotawaliwa na teknolojia.
Dkt.Bilal ametoa rai hiyo mwishoni mwa
wiki wakati akipokea msaada wa vifaa vya ujenzi kumalizia ujenzi wa kituo cha
uendelezaji n a u k u z a j i ma t umi z i ya Tehama cha Shule ya Msingi
Kisiwandui pamoja na kompyuta kumi kwa ajili ya kituo cha kompyuta cha kijamii
cha Chwaka vyote vya Mjini Zanzibar vilivyotolewa na Mfuko wa Kampuni ya
Vodacom wa kusaidia jamii vyenye thamani ya sh.milioni 23.
Makamu wa Rais alisema uwekezaji kwenye
Tehama ni moja ya mambo yanayopaswa kupewa kipaumbele kwa wakati huu hasa kwa
vijana ambao hawana sababu ya kuishi nje ya mfumo na zama zinazotawaliwa na matumizi
makubwa ya teknolojia katika kila nyanja ya maisha ikiwemo mfumo rasmi wa
elimu.
Alisema maisha ya sasa yanahitaji
kompyuta na Tehama kwa kiaisi kikubwa na hivyo kuipongeza Vodacom Foundation
kwa kuona umuhimu wa kusaidia vituo hivyo viwili msaada ambao ni wa wakati na
wa umuhimu kulingana na mahitaji ya wakati.
"Viongozi wa ngazi zote za
Serikali tuweke ajenda ya Tehama ili kuviwezesha vizazi vya sasa kuishi na
wakati wao," alisema na kuongeza kuwa
"Sisi tuliozaliwa na kukulia
katika zama za BBC (Born Before Computer) tunapoona mapinduzi haya makubwa ya
kiteknolojia tunakumbuka tulipotoka na tunawaza ni vipi maisha yatakuwa katika
miaka michache ijayo kutokana na ukuaji wa kasi wa matumizi ya Tehama.
"Tunachotaka ni kuona vijana ambao
ndiyo wa kizazi cha Tehama wasiulize wanachokitaka leo bali wajiulize na kupata
suluhu ya nini kitakachohitajika miaka ijayo na ili tufikie huko ni lazima
tuwaandae vijana na tuwekeze kisawasawa kwenye Tehama na kutokana na hilo basi
ndiyo maana nawashukuru sana Vodacom kwa kuona umuhimu wa Tehama kwa jamii na
kutoa misaada hii.
"Kila kitu siku hizi kipo kwenye
mtandao hakuna haja ya kusumbuka kama ilivyokuwa wakati wetu ambapo mwalimu kwa
mfano alilazimika kutumia muda mwingi sana kusoma kitabu kizima ili kupata notisi
za kufundishia darasani, lakini sasa kila kitu ni kudadavua tu," alisema.
D k t . B i l a l a m b a y e alitumia
muda mwingi kuelezea utofauti wa maisha yalivyokuwa enzi za bila ya kompyuta na
hali ilivyo hivi sasa aliwaomba wadau wengi zaidi kujitokeza na kusaidia juhudi
za ukuzaji na uendelezaji wa matumizi ya Tehama kwa vijana ili kuwalinda vijana
hao kutoishi kizamani.
Kwa u p a n d e wa k e Mwenyekiti wa
Bodi ya Vodacom Foundation Hassan Saleh alisema muono wa Vodacom ni kuona kila
Mtanzania anafikiwa kwa urahisi na huduma za intaneti ili kuweza kunufaika na
mapinduzi ya kiteknolojia yanayotokea ulimwenguni.
"Nia ya kampuni ya Vodacom ni kuona kila Mtanzania
anafikiwa na huduma za intaneti na kuwa na uwezo wa kuzitumia kwa kuwa
tunatambua umuhimu wake kwa maisha ya watu na maendeleo yao kwa sasa bila
kujali aina ya kazi au kipato na ndiyo maana tumejitoa kusaidia vituo hivi
vinavyoleta huduma za Teham
No comments:
Post a Comment