19 August 2013

MENGI MWENYEKITI MPYA WA BODI YA TPSPWAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa 14 wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) wamemchagua Mwenyekiti wa kampuni za IPP, Dkt. Reginald Mengi, kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya taasisi hiyo katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki, anaripoti Mwandishi Wetu.

Uchaguzi huo mkuu ulikuwa ni sehemu ya mkutano mkuu wa mwaka, ambapo taasisi hiyo ilitumia fursa hiyo kufanya uchaguzi wa kupata bodi mpya baada ya bodi iliyokuwa ikiongozwa na Esther Mkwizu kumaliza muda wake.
Uchaguzi huo ulioendeshwa kwa njia ya kura ulisimamiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo. Wajumbe wa mkutano mkuu waliopiga kura walikuwa 73 ambapo Dkt. Mengi alipata kura 39 huku mgombea mwingine, Salum Shamte, akipata kura 34.
“Kulingana na sheria ya taasisi hii aliyepata kura nyingi anakuwa mwenyekiti mpya wa bodi ya wakati aliyepata kura pungufu anakuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi,” alisema, Mapunjo alipokuwa akitangaza matokeo hayo.
Kwa maana hiyo, Salum Shamte anakuwa Makamu Mwenyekiti mpya.
Viongozi hao wapya watahudumu katika nafasi hizo kwa muda wa miaka miwili na baada ya kumaliza wanaweza kuingia katika uchaguzi tena kuomba ridhaa ya kuongoza katika kipindi cha pili.
Mkutano huo mkuu pia uliwachagua wajumbe 11 walioomba uongozi kupitia kongano wanazotoka ili kuwa wajumbe wa bodi hiyo.
Wa j u m b e w a b o d i waliochaguliwa ni pamoja n a De o d a t u s Mwa n y i k a atakayewakilisha kongamano ya Nishati na Madini, Felix Mosha (Uzalishaji, Viwanda), Enock Dondole (vikundi vya biashara mikoani), Anna Matinde (wajasiriamali wanawake), Mbarouk Omar (Taasisi ya Sekta Binafsi Zanzibar).
Wengine ni Eng.Peter Chisawillo (Biashara), Bw. Salum Shamte (Kilimo), Bw. Gaudence Temu (Rasilimali na Utalii), Dkt. Gideon Kaunda (Makampuni), Dkt. Charles Kimei (Benki na huduma za kifedha) na Dkt. Reginald Mengi (huduma).

No comments:

Post a Comment