Na Florah
Temba, Moshi
MENEJA wa Benki ya CRDB, Tawi la Moshi,
mkoani Kilimanjaro, Bw. Francis Mollel (56), amefikishwa kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kwa kosa la kumdhalilisha mteja kijinsia ndani
ya benki hiyo jambo ambalo ni kiunyume cha sheria.
Mbele
ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kilimanjaro, Timosetheus Swai, wakili wa
Serikali, Bw. Patrick Mwita, alisema mshtakiwa huyo anatuhumiwa kutoa maneno ya
udhalilisha kijinsia kwa mteja aliyefahamika kwa jina la Lulu Kajembe ambaye
aliwahi kuwa mfanyakazi wa benki hiyo.
Ilidaiwa kuwa, Juni
Mosi mwaka huu ndani ya benki hiyo, Tawi la Moshi, mshtakiwa alitoa maneno ya
udhalilishaji kwa mteja aliyekuwa kwenye foleni akisubiri kupata huduma za
kibenki.
Mshtakiwa alikana
shtaka hilo ambapo dhamana yake ilikuwa wazi hivyo alitakiwa kuwa na wadhamini
wawili, mmoja kutoka taasisi inayotambulika kisheria.
Hakimu Swali,
alimuachia mshtakiwa huyo kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ambayo ni
pamoja na kutoa sh. milioni moja.
Sharti lingine ni
kutotoka nje ya Mkoa huo, kuwasilisha hati ya kusafiria na kama atahitaji
kusafiri nje ya Mkoa awasilishe maombi mahakamani.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 21, mwaka huu ambapo
itakuja mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa
Hilo nalo neno....maboss mna kazi!
ReplyDeleteSwala la customer care bado ni tatizo kubwa katika sekta mbalimbali hapa nchini..Hii ni changamoto ambayo watanzania tunatakiwa kuifanyia kazi.Lakini pia maadali ya kazi nayo hayazingatiwi ipasavyo haswa kwa watu wa nyadhifa za juu katika sekta mbalimbali.Kama tunataka kuendelea ni vyema tubadilike
ReplyDelete