16 August 2013

MENEJA CRDB MOSHI KIZIMBANI Na Florah Temba, Moshi
MENEJA wa Benki ya CRDB, Tawi la Moshi, mkoani Kilimanjaro, Bw. Francis Mollel (56), amefikishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kwa kosa la kumdhalilisha mteja kijinsia ndani ya benki hiyo jambo ambalo ni kiunyume cha sheria.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kilimanjaro, Timosetheus Swai, wakili wa Serikali, Bw. Patrick Mwita, alisema mshtakiwa huyo anatuhumiwa kutoa maneno ya udhalilisha kijinsia kwa mteja aliyefahamika kwa jina la Lulu Kajembe ambaye aliwahi kuwa mfanyakazi wa benki hiyo.
Ilidaiwa kuwa, Juni Mosi mwaka huu ndani ya benki hiyo, Tawi la Moshi, mshtakiwa alitoa maneno ya udhalilishaji kwa mteja aliyekuwa kwenye foleni akisubiri kupata huduma za kibenki.
Mshtakiwa alikana shtaka hilo ambapo dhamana yake ilikuwa wazi hivyo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja kutoka taasisi inayotambulika kisheria.
Hakimu Swali, alimuachia mshtakiwa huyo kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ambayo ni pamoja na kutoa sh. milioni moja.
Sharti lingine ni kutotoka nje ya Mkoa huo, kuwasilisha hati ya kusafiria na kama atahitaji kusafiri nje ya Mkoa awasilishe maombi mahakamani.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 21, mwaka huu ambapo itakuja mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa

2 comments:

  1. Hilo nalo neno....maboss mna kazi!

    ReplyDelete
  2. Swala la customer care bado ni tatizo kubwa katika sekta mbalimbali hapa nchini..Hii ni changamoto ambayo watanzania tunatakiwa kuifanyia kazi.Lakini pia maadali ya kazi nayo hayazingatiwi ipasavyo haswa kwa watu wa nyadhifa za juu katika sekta mbalimbali.Kama tunataka kuendelea ni vyema tubadilike

    ReplyDelete