Na Mwandishi Wetu
BARAZA la Habari Tanzania (MCT)
limeandaa Mkutano wa Kitaifa wa Baraza la Katiba la Tasnia ya Habari
utakaofanyika kesho Jijini Dar es Salaam ili kupokea maoni ya mwisho ya wajumbe
yaliyotokana na majumuisho ya mikutano ya kikanda ya Baraza la Katiba la Tasnia
ya Habari
Katibu Mtendaji
wa MCT, Kajubi Mukajanga, alisema MCT iliratibu mikutano ya Baraza la Katiba la
Tasnia ya Habari iliyofanyika katika kanda sita ambapo jumla ya wajumbe 143
walishiriki kutoa maoni yao
juu ya Rasimu ya Katiba.
Tume ya
Mabadiliko ya Katiba ililitambua rasmi Baraza la Katiba la Tasnia ya Habari
kuwa mojawapo ya Mabaraza ya Katiba kulingana na kifungu cha 18 (6) cha Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, ambapo Tume inaweza kuruhusu asasi,
taasisi na makundi ya watu wenye malengo yanayofanana kuunda Mabaraza ya
Katiba.
Mukajanga alisema wajumbe wa Baraza la
Katiba la Tasnia ya Habari wanatokana na wanachama wa MCT ambao wanakidhi sifa
zilizoainishwa kwenye Mwongozo wa Kupata Wawakilishi wa Mabaraza ya Katiba
uliotolewa na Tume.
Sifa mahsusi ikiwa ni pamoja na kuwa
ofisa mwandamizi kwenye taasisi husika na mwanahabari. Mkutano wa Kitaifa wa
Baraza la Katiba la Tasnia ya Habari utawakutanisha wajumbe ambao ni wanachama
wa Baraza la Habari Tanzania walioshiriki katika mikutano ya ngazi ya kanda kwa
ajili ya kupokea maoni yao ya mwisho yaliyofanyiwa majumuisho.
Kanda zilizohusika kuendesha mikutano
hiyo ni pamoja na Kanda ya Kaskazini, Ziwa Victoria, Nyanda za Juu Kusini, Dar
es Salaam, Kati na Kanda ya Zanzibar.
Mikutano ya kikanda imesaidia kupata
maoni, mawazo, michango n a map endek ez o amb ayo yamechambuliwa na
yatapelekwa kwenye Mkutano wa Kitaifa kwa ajili ya mjadala na uchambuzi zaidi.
Mukajanga alisema maoni n a m a p e n d e k e z o m a p y a yatakayotolewa
kwenye Mkutano wa Kitaifa yatajumuishwa kwenye andiko moja na yale ya kikanda.
Andiko hilo litaandaliwa na MCT kwa kushirikiana na wataalamu na kuwasilishwa
rasmi kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba kama ilivyoelekezwa na Tume.
No comments:
Post a Comment