19 August 2013

MAMLAKA ZA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA ZIWAJIBIKENa Rehema Maigala
MA M L A K A zenye wajibu wa k u p amb a n a n a dawa za kulevya zimetakiwa kuwajibika ipasavyo kutokana na Tanzania kugeuka kitovu cha biashara ya dawa hizo.Ta a r i f a i l i y o t umwa kwenye vyombo vya habari na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, mwi s h o n i mwa wi k i ilisema vijana wa Tanzania wamekuwa wakikamatwa maeneo mbalimbali duniani wakihusishwa na biashara ya dawa za kulevya.

Alisema kuwa njia moja wapo ya kupambana na uharamia huo ni uwajibikaji wa mamlaka zenye wajibu huo.Hata hivyo, alisema Kamati za Bunge zinawajibu wa kuhoji mahesabu ya mamlaka hizo kuhusiana na matumizi ya fedha za umma zinazotengwa kupambana na biashara ya dawa za kulevya kwani biashara hiyo inazidi kushamiri
Alisema kuwa iwapo tutawajibisha Wizara ya Mambo ya Ndani kitengo cha kupambana na dawa za kulevya."Hatuwezi kuwa tunatenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kupambana na biashara hii haramu lakini bado inazidi kushamiri kila mwaka, ni lazima kila mwenyewajibu awajibishwe," alisema.
Aliongeza kuwa Kamati za Bunge za Mahesabu ni asasi muhimu za demokrasia k w a n i h u s i m a m i a uwajibikaji ni vyema kamati hizi kupewa uzito stahili kwa kuwa na rasilimali za kutosha za kufanya kazi zake na kuhakikisha taarifa zake zinapata uzito katika utekelezaji.
 Alisema kimsingi Kamati zote za Bunge ni sawa kihadhi lakini Kamati za mahesabu ndiyo Bunge kiuhalisia. P i a a l i s ema k a t i k a kutekeleza wajibu, ni muhimu na lazima wajumbe wa kamati kujiepusha na vitendo vya rushwa kwani vitendo hivyo huzuia usimamizi na hatimaye kuendeleza rushwa kwa wanaosimamiwa uwajibikaji ni silaha dhidi ya rushwa na hivyo wanaosimamia uwajibikaji ni lazima wawe wasafi.
Alisema kuna wigo mdogo wa kodi wakati zinatumika fedha nyingi kukusanya kodi hiyo kidogo hivyo ni wajibu wa kamati kuona kwamba ufanisi katika kukusanya kodi unafikiwa ikiwemo kuzuia mianya ya ukwepaji wa kodi.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), asilimia 15 ya makusanyo hayakusanywi kwenye idara ya mapato peke yake kutokana na ukwepaji wa kodi hiyo ni takriban sh. 490 bilioni kwa kutumia makadirio ya mwaka wa fedha 2012/13.

No comments:

Post a Comment