16 August 2013

MCHAKATO WA UCHAGUZI TFF KUTANGAZWA LEONa Mwandishi Wetu
MCHAKATO wa Uchaguzi wa kamati mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), unatarajiwa kutangazwa leo.Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho hilo, Hamidu Mbwezeleni mbali ya kutangaza mchakato utakavyokuwa pia atangaza tarehe ya uchaguzi.

Uchaguzi Mkuu wa TFF ulipangwa kufanyika Septemba, mwaka huu lakini uliahirishwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), kutokana na baadhi ya wagombea kulalamika kuenguliwa kugombea.
"Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilikutana Jumapili (Agosti 11 mwaka huu) na inatarajia kuwa na kikao kingine leo (jana) ambapo pamoja na mambo mengine itazungumzia maandalizi ya uchaguzi huo," alisema.Mbali ya Mbwezeleni, wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti), Mohamed Sinani, Chabanga Dyamwale na Kitwana Manara

No comments:

Post a Comment