05 August 2013

MAFISADI WAOMBEWA ADHABU


Na Goodluck Hongo
SERIKAL I imet aki wa kuanzishamfumo mpyawakuwataja nak uwafich uawatuwanaotumi anafasiza o za kazikutafun a fedhaza umma na kujin ufaishabinafsi.Akizu ngumzana M ajira Dar es Salaamjana, Ka tibuMtendaji waKitu ochaUta fitina U badhirifuwaM ali zaUm ma(CFRI,) An dendek isyeMw akabalulaalisema nivyemaSerik aliikaanzisha mfumohuowak uwat ajawa tuwanao tumianafa si z akazikati kaku tafunafedha za umma.

Sambamba na kujinufaisha binafsi ingawa Serikali inajitahidi ku pambanana watumishi ambao siwaadilifu.
Al isema, k uanziamwaka 2006hadi sasaserikali imefanyama boreshomengi ka tikakupam bana nawatumis hi wasiowaad ilifukatikanafasizaoz akazik uan zishwakwa kamat i za b unge zakusima miahesa bu za se rikalia mbazozimel eta tijakubwakatika uwajib ikajinauwazi katika matumizi ya pesa za umma.
A lisema , mbal i na hiyolakini piaSheriaMpyayaKupa mbanana Ru shway am waka2007nayaukagu ziw arasilim ali za ummayamwaka2008amb azonazo k wa pamoja zime letatija katika kupambana na watumishi wanaotumia nafasi zao za kazi kwa manufaa yao.
“Katika ripoti ya tathmini ya mwenendo wa upambanaji wa rushwa Tanzania iliyotolewa mwaka 2011 kwa kushirikisha mataifa mbalimbali kama DFID, SADEV, ADB, Sida, Danida pamoja na Norway inaonesha kuwa Tanzania imepiga hatua katika kupambana na rushwa kutoka kupata alama D+ mwaka 2005 mpaka alama C+ mwaka 2008,”alisema Mwakabalula.
Aliongeza kuwa, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ameifanya Tanzania kuwa katika kiwango cha kimataifa katika udhibiti na ukaguzi zaidi mpaka kufikia kiwango cha kwanza katika ukaguzi ambao unatambulika kimataifa (Level 1 of AFROSAI-E) lakini pamoja na jitihada zote hizo bado watumishi wanazidi kutumia nafasi zao za kazi katika kujinufaisha wenyewe.
Alibainisha kuwa, hali hiyo ya kutumia fedha za umma inatokana na mfumo ambao watumishi hao hawaogopi kwa sababu wanaona kuwa hamna mfumo ambao utawawajibisha kikamilifu mbele ya jamii na familia yake huku wakati mwingine serikali ikishindwa kuyafanyia kazi mapendekezo yanayotolewa na CAG.

No comments:

Post a Comment