05 August 2013

WAFANYAKAZI TTCL WATAKIWA KUCHAPA KAZI KWA MAARIFA


Na Rachel Balama
WATUMISHI wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wametakiwa kuongeza juhudi, umoja na maarifa ili kuhakikisha wanafanya kampuni hiyo inakuwa ya mfano wa kuigwa ndani na nje ya nchi.Ushauri huo ulitolewa na aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Kampuni wa TTCL, Gilder Kibola, wakati akizungumza na wafanyakazi na menejimenti ya kampuni hiyo kwenye hafla ya kumuaga mwishoni mwa wiki Dar es Salaam.
Alisema ni muhimu kwa wenzake wanaobaki kuendeleza juhudi na kumpa ushirikiano Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo ili aweze kufikia malengo yake.

"Nawashauri muendelee kumpa ushirikiano kiongozi wetu ili malengo yake aweze kufikiwa," alisema. Kibola alisema kufanikisha mipango na malengo ya kampuni hutegemea ushirikiano na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu yake.Kibola alijiunga na kampuni hiyo mwaka 1996 akiwa kama Afisa Sheria na kupanda ngazi hadi kufikia nafasi hiyo ambayo amestaafu nayo.
" N i n a s h u k u r u Mu n g u namaliza salama na afya njema, nimejifunza mengi naomba vijana katika kampuni hii kuhakikisha mnajifunza kwa waliowatangulia utendaji kazi mzuri kwa kuzingatia busara na weledi," alisema" J i f u n z e n i k w a w a t u wa l i owa t a n g u l i a k a z i n i , mtafanikiwa," alisema.Ofisa Mkuu Mtendaji wa TTCL, Dkt. Kamugisha Kamuzora, alisema kampuni itamkumbuka kwa mchango wake wa uchapaji kazi.
Mkuu wa utumishi wa Kampuni hiyo, Juvenal Utafu alisema, Kibola amekuwa pamoja na kampuni katika vipindi mbalimbali vilivyopitiwa na TTCL na hakutetereka hadi anastaafu kwa heshima.Aliongeza kwamba alikuwa kiungo muhimu kati ya wafanyakazi na bodi na amechangia mafanikio katika idara ya sheria.

No comments:

Post a Comment