30 August 2013

LHRC YATOA MAPENDEKEZO RASIMU YA KATIBA



Na Leah Daudi
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimewasilisha maoni yake ya katiba mpya ambapo kimependekeza kushika wadhifa huo kwa vipindi vitatu vya kukaa. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurungenzi Mtendaji wa LHRC, Dkt. Helen -Kijo Bisimba, alisema kituo kimechambua vifungu vyote na kuainisha masuala mbalimbali ambayo yanahitajika kurekebishwa.

Alisema kuwa pamoja na kuchambua vifungu mbalimbali aliyataja mambo ambayo yanahitajika kuendelea kuwepo kama vile makundi maalumu ya wazee, vijana na watoto. "Tumefanya hivyo kwa kuigawa rasimu katika dhima kuu nane, ambazo ni mambo ya jumla na masuala ya mtambuko haki za binadamu, utawala wa Serikali Bunge, Mahakama, Muungano, Vyombo vya Katiba na Taasisi za uwajibikaji na uchaguzi na vyama vya siasa," alisema Bisimba.
Alisema wanataka usawa uwepo wa wanawake na wanaume bungeni ili kuweza kuwa na haki sawa kwa wananchi. Alitaja mambo ya kurekebisha katika Rasimu hiyo ikiwa ni pamoja na haki za binadamu kuwa na ulinzi wa kutosha pamoja na adhabu ya kifo kufutwa nchini.

1 comment:

  1. JE SABABU ZA TANZANIA KUACHA KURIDHIA TAMKO LA HAKI ZA BINADAMU LA UMOJA WA MATAIFA BADO SABABU ZILE BADO ZINAKIDHI MAHITAJI YA WAKATI WA LEO TUSIPOKUWA NA RASILIMALIWATU YA KUTABIRI KESHO ITAKUAJE NI HATARI SANA KWANI TULIYO NAYO NI ILA RASILIMALIWATU TULIYONAYO NI ILE ILIYOSHANGAA JUZI IKITOKEA WALA SI JANA

    ReplyDelete