Na Ester Maongezi
MAMLAKA ya Mapato Ta n z a n i a ( T R A ) imesema kuanzia
sasa itakuwa inapokea taarifa moja kwa moja kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania
juu ya mizigo inayoingia na kutoka ili kuondoa tatizo la udanganyifu uliokuwa
ukifanywa na wafanyabiashara na watendaji. Hatua hiyo inalenga ukwepaji ulipaji
kodi
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Ofisa Elimu Idara ya Kodi wa
TRA, Richard Kayombo, wakati akizungumza na waandishi wa gazeti hili. Alisema kwa kipindi cha nyuma taarifa zilikuwa zinaenda bandarini
kwanza na wao kupewa taarifa tu mzigo unapotoka jambo ambalo lilikuwa likiwapa
shida wakati wa ufuatiliaji na ukaguzi.
Kayombo alisema ilikuwa ikiwapa shida kwasababu ya
kutokushirikishwa katika kipindi cha mizigo inapoingia bandarini kitu ambacho
kilichangia sana wao kutokupata taarifa sahihi. "Kwa sasa TRA tunapata taarifa mapema kabla ya mzigo
kushushwa kitu amabcho kinatusaidia kujua kontena linakuwa na mzigo wa aina
gani na wenye thamani ya kiasi gani," alisema Kayombo.
Katika hatua ya kuboresha m a p a t o , TRA i m e z i n d u a
mfumo mpaya wa udhibiti wa bidhaa katika bandari ya Dar es Salaam ujulikanao
kama Cargo Management System ili kuboresha na kurahisisha uondoshaji wa bidhaa
banadarini na ubadilishanaji habari kati ya watendaji.
Kayombo alisema anaamini mfumo huu mpya ulioanza tangu Agosti 14,
utasaidia kuweka rekodi za bidhaa zinazoingia nchini na unaziwezesha mamlaka
hizo kufuatilia taarifa kwa ufanisi zaidi, pia kuzuia wizi wa bidhaa kutoka
bandarini.
Aliongeza kuwa mfumo huo utawawezesha mawakala wa meli kutuma
taarifa ya bidhaa kwa idara ya Forodha wakiwa mahali popote penye mtandao, pia
utasaidia kulinda ushuru na kodi za Serikali na mali za wateja kwa ufanisi
zaidi.
Kayombo alitoa mwito
kwa wadu wengine kutoa ushirikiano na kuimarisha mifumo yao ili iwe rahisi kubadilishana taarifa na
idara ya Forodha huku akisema kuwa endapo kutakuwa na hitilafu zozote basi
wananchi wasisite kuwasiliana na TRA.
No comments:
Post a Comment