Na Rachel Balama
WAPINGA rufaa katika k
e s i y a ma u a j i y a w a f a n y a b i a s h a r a iliyokuwa ikimkabili
aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe na askari
wenzake wanane walioachiwa huru katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa
madini wameiomba Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kupewa muda ili
kuwasilisha majibu ya maombi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ya
kuongezewa muda wa kukata rufaa.
Akiwasilisha maombi hayo mbele ya Jaji Aloyisius Mujuluzi, wakili
wa wapinga rufaa Majura Magafu, aliiomba wapewe muda ili waweze kuwasilisha
majibu dhidi ya DPP. Alisema kuwa walichelewa kupata maombi ya DPP dhidi ya wateja wao
kwa kuwa maombi hayo yalitumwa moja kwa moja kwa wateja wao.
"Mheshimiwa Jaji, tunaaomba muda wa kuwasilisha majibu yetu
kwa kuwa, upande wa Serikali uliwatumia moja kwa moja wateja wetu ndipo wateja
hao walitutumia sisi," alisema Magafu.
Mbali na Magafu wapinga rufaa hao pia wanatetewa na mawakili
Richard Rweyongeza na Dennis Msafiri.
Akijibu hoja hiyo wakili upande wa Serikali, Timoth Vitalis,
alisema kuwa hawana pingamizi na hoja hiyo. Hata hivyo Jaji anayesikiliza rufaa
hiyo, aliutaka upande wa wapinga rufaa kuwasilisha majibu yao Septemba 2, mwaka
huu ambapo na upande wa serikali uwasilishe majibu Septemba 4, mwaka huu.
Jaji aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 5, mwaka huu ambapo
mahakama itaanza kisikiliza. DPP aliwasilisha maombi mahakamani ya kuongezewa muda wa kukata
rufaa, baada ya mahakama ya Rufaa ya Tanzania kutupilia mbali rufaa ya awali
kwa sababu ilikuwa na makosa kisheria. Rufaa hiyo ilitupwa baada ya kubaini kuwapo kwa dosari katika hati
ya kusudio la kukata rufaa na mahakama kukataa kuamuru makosa yaliyojitokeza
yafanyiwe marekebisho.
Katika shauri hilo mbali na Zombe wajibu rufaa wengine ni askari
Christopher Bageni, Ahmed Makele, Jane Andrew, Koplo Emmanuel Mabula, Michael
Shonza, Abeneth Saro, Rajabu Bakari na Festus Gwasab.
Serikali ilikata rufaa hiyo kupinga hukumu iliyotolewa Agosti, 17,
mwaka 2008 na Mahakama Kuu, Kanda ya Dar
es Salaam iliyowaachia huru.
No comments:
Post a Comment