22 August 2013

KILI MUSIC TOUR KUHAMIA MBEYA



 Na Mwandishi Wetu
TAMASHA la Kili Music Tour, linatarajiwa kuhamia jijini Mbeya ambapo Jumamosi hii, litafanyika katika Uwanja wa New City Pub.Ta m a s h a h i l o a m b a l o limeshafanyika katika baadhi ya mikoa, linatarajiwa kurindima Mbeya kwa kushirikisha wasanii tisa wa muziki wa kizazi kipya pamoja na hip hop.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema tamasha hilo linatarajiwa kuwa la aina yake kutokana na maandalizi waliyoyafanya
.Alisema maandalizi kwa kiasi kikubwa yameshafanyika, ambapo pia mashabiki wa muziki mkoani humo watapata fursa kusikia nyimbo mpya za wasanii, watakaoshiriki kwenye tamasha hilo.Aliwataja wasanii watakaoshiriki kwenye tamasha hilo kuwa ni Linex, Fid Q, Barnaba, Prof J, Kala Jeremiah, Ben Paul, Izzo Biz, Snura pamoja na Awilo wa Mbeya.
"Tunashukuru kuwa Watanzania wamepokea tamasha hili kwa moyo mkunjufu kabisa na walishiriki kikamilifu kwenye mikoa ya Dodoma, Tanga, Kilimanjaro na Mwanza," alisema Kavishe.Kavishe alisema lengo kubwa la tamasha hilo ni katika kuondoa dhana ya Watanzania, kwamba kila kitu kinafanyika Dar es Salaam, hivyo anategemea Mbeya itajumuika nao ipasavyo.
Kwa niaba ya wasanii wenzake msanii mahiri wa muziki wa hip hop, Fareed Kubanda 'Fid Q' amewataka wakazi wa Mbeya kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya New City Pub."Tumejiandaa vizuri kutoa burudani kali, ambapo mashabiki watakaojitokeza watapata fursa ya kusikia baadhi ya nyimbo ikiwa ni pamoja na zile mpya ambazo hawajawahi kuzisikia," alisema

No comments:

Post a Comment