16 August 2013

KIIZA APATA ULAJI LEBANONNa Elizabeth Mayemba
MSHAMBULIAJI wa Yanga raia wa Uganda, Hamis Kiiza anatarajiwa kwenda Lebanon kwa ajili ya kufanya majaribio katika klabu moja ya huko.Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, alisema Dar es Salaam jana, mara baada ya mechi ya kesho ya Ngao ya Jamii kati ya timu hiyo na Azam FC, siku inayofuata, Kiiza atakwenda Lebanon na akifuzu majaribio atasajiliwa moja kwa moja.

"Kuna ofa nzuri imeletwa kutoka Lebanon, hivyo mara baada ya mechi yetu na Azam FC, Kiiza kesho yake ataondoka kwenda kufanya majaribio kwenye moja ya klabu ya huko Lebanon," alisema kiongozi huyo.Alisema ofa iliyoletwa ni nzuri na hawawezi kumbania mchezaji huyo kwa kuwa naye anatafuta maisha, hivyo akifaulu majaribio yake watamuuza katika klabu hiyo.
Kiongozi huyo alisema klabu hiyo inayomtaka, Kiiza imefuata taratibu zote na wao kama viongozi wametoa baraka kwa mchezaji huyo na kumtakia mafanikio mema, ili aweze kufuzu majaribio yake.
Endapo Yanga wasingefikia makubaliano na mchezaji huyo, wangejikuta wanapoteza fedha nyingi za usajili kwa kuwa tayari alikuwa ameshamaliza mkataba wake na klabu hiyo.
Kiiza alikuwa akitaka klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani, imlipe fedha zote za usajili kwa mkupuo, ambapo kila mkataba ulikuwa ni dola za Marekani 40,000 hivyo kwa miaka miwili alitaka alipwe dola 80,000.Hata hivyo baadaye klabu hiyo ilikubaliana na mchezaji huyo na kusaini tena mkataba mpya wa miaka miwil

No comments:

Post a Comment