13 August 2013

POLISI WATANGAZA DONGEFrank Monyo na Theophan Ng’itu
JESHI la Polisi Kanda ya Dar es Salaam limeahidi kutoa zawadi nono ya kitita cha sh. milioni 100 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa za wahalifu wanaotumia tindikali. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini, Kamishna wa Polisi katika kanda hiyo, Suleiman Kova alisema kuwa kutokana na matukio ya watu kumwagiwa tindikali kuongezeka, Jeshi la Polisi limejipanga kudhibiti hali hiyo.“Kutokana na vitendo hivi vya uhalifu kuongezeka tunaomba wananchi wasaidiane na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za wahalifu kupitia namba yangu 0754034224 au wanione (Kova) ofisini kwangu moja kwa moja”,alisema Kova.

No comments:

Post a Comment