13 August 2013

YANGA KUJICHIMBIA PROTEA KESHONa Mayasa Mariwata
KIKOSI cha Yanga kinatarajia kuingia kambini kesho, kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC itakayopigwa Jumamosi pamoja na Ligi Kuu ya Vodacom itakayoanza Agosti 24, mwaka huu.

Yanga kwa sasa inafanya mazoezi katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola Mabibo, Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu Erne Brandts na msaidizi wake Fred Minziro.Akizungumza Dar es Salaam jana mmoja wa viongozi wa klabu hiyo, ambaye hakupenda kuandikwa jina lake gazetini alisema kikosi hicho kitajichimbia katika hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay, Dar es Salaam.
"Wachezaji wote wataingia kambini kesho ili kujiimarisha zaidi, kwani ligi inakaribia kuanza na pia tunajiandaa na Azam FC katika mechi yetu ya Ngao ya Jamii," alisema kiongozi huyo.Lakini Ofisa Habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto, alipotakiwa na mwandishi wa habari hizi kuzungumzia kuhusu kambi hiyo alisema, bado hajapata uhakika juu ya suala hilo na hawezi kulielezea. "Sina uhakika na hilo, hivyo ni ngumu kulielezea mpaka pale nitakapopewa taarifa," alisema.

No comments:

Post a Comment