07 August 2013

MGANGA AUWAWA KIKATILI


Na Eliasa Ally, Iringa
MGANGA wa jadi, George Tereva (55) mkazi wa Kijiji cha Lungemba wilayani Mufindi Mkoa wa Iringa ameuawa kikatili baada ya watu wasiojulikana kwenda nyumbani kwake na kupiga risasi tatu katika maeneo ya tumboni, kichwani na kwenye paji lake la uso.Pia watuhumiwa hao walimcharanga mganga huyo kwa panga kichwani na kutoweka bila kuchukua mali zozote za marehemu huyo
.Akizungumzia tukio hilo ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi alisema tukio hilo la kusikitisha lilitokea Augosti 4, mwaka huu, saa 1:30 usiku katika Kijiji cha Lugemba.Kamanda huyo alisema, tukio hilo lilitokea baada ya watu wawili wasiojulikana kumvamia nyumbani kwake na kuanza kumfyatulia risasi hadi kuuondoa uhai wake ambapo pamoja na kumuua kwa risasi waliendelea kumcharanga kwa panga.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Waganga wa Jadi Mkoa wa Iringa, Dkt. Galus Msekwa akizungumzia tukio la kuuawa kwa mganga mwenzao, George Tevere ambaye alikuwa anawatibu wagonjwa kimeisikitisha jumuiya yao mkoani humo.
"Watu walikwenda kwa mganga huyo kuomba gari kwa malengo ya kutaka wasafirishiwe mgonjwa wao hadi anapoishi mganga huyo, lakini alipotoka ndani ya nyumba ili awasikilize ndipo walipoanza kumshambulia kwa kumpiga risasi tumboni;"Kichwani na baadaye kuanza kumcharanga kwa mapanga katika maeneo ya mwili wake hasa kichwani hadi kusababisha kifo chake, suala hili limetushtua sana," alisema Dkt. Msekwa.

No comments:

Post a Comment