BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) Kanda ya
Kaskazini, Arusha imewatahadharisha wananchi kuhusiana na tatizo la noti bandia
nchini, anaripoti Richard Konga, Arusha.Akizungumza wakati wa Maonesho ya
Wakulima Nane nane yaliyomalizika hivi karibuni, Meneja wa Fedha na Utawala wa
BoT, Evena Ndesingo, alisema benki hiyo imeanza kutumia maonyesho ya wakulima
kutoa elimu ya utambuzi wa noti zake
. Alisema wananchi wanatakiwa kuwa makini
wakati wa kutoa au kupokea fedha ili kuepuka kufilisika na kuyumbisha uchumi wa
taifa.“Benki imeanzisha utaratibu wa kutoa
elimu kwa wananchi ili watambue noti bandia kupitia alama halisi zilizoko
kwenye noti halali,” alisema.
Hata hivyo, alisema matumizi ya noti
bandia ndani ya jamii yanapungua kila mwaka kutokana na jamii kuwa na uelewa wa
noti halisi na bandia na hivyo kupunguza kasi ya mzunguko wa noti bandia hizo.
Alisema BoT kupitia matawi yake nchini
imejidhatiti kuwaelimisha wananchi juu ya utambuzi wa noti mpya na alama zake
ili jamii izielewe na kutofautisha noti hizo.Alisema noti bandia iwapo zitaachwa ziendelee
kuwepo kwenye mzunguko wa matumizi ya kawaida ipo hatari kwa jamii kufilisika
na taifa kuyumba kiuchumi.
Ndesingo aliwataka wananchi kuwa makini wanapofanya malipo
ya noti mpya kwa kuchunguza kwa makini alama hizo kabla hazijapelekewa matumizi
ya noti hizo kwa mtu mwingine.
No comments:
Post a Comment