02 August 2013

AZAM FC KWENDA SOUTH KESHONa Mosi Mrisho
TIMU ya Azam FC inatarajia kuondoka nchini leo kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF)
.Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha Mkuu wa Azam FC Stewart Hall alisema kuwa, wakiwa Afrika Kusini watacheza mechi nne ambapo mechi ya kwanza watacheza na Bloemfontein Celtic ambayo itafanyika Agosti 6, mwaka huu kwenye jimbo la Free State.
Hall alisema kuwa mechi nyingine zitakuwa dhidi ya timu maarufu kama Orando Pirates, Super Sports United na Amazulu ambazo tarehe zake zitatangazwa baadaye.
Alisema kuwa lengo lao kubwa la ziara hiyo ni kujiwekea nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara baada ya kutwaa nafasi ya pili kwa miaka miwili mfululizo.
"Tumetosheka na nafasi ya pili na sasa tunataka kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara, hiyo ndiyo nia yetu kubwa, timu imeanzishwa miaka michache iliyopita na imekwisha weka historia katika nchi hii na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, tunataka kuweka historia mpya," alisema Hall
Alisema wamepania kufanya mambo makubwa katika msimu huu na ndiyo maana wameamua kutosajili wachezaji wapya kutokana na kurejea kwa Aggrey Morris, Erasto Nyoni na Said Mourad
.
.

No comments:

Post a Comment