02 August 2013

TANZANIA BINGWA WA DUNIA KURUKA KAMBA




Mshindi wa Ubingwa wa Dunia wa mchezo wa kuruka kamba huko Marekani, Mtanzania Hamisi Mohammed Kondo akionesha kipaji chake kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), uliofanyika Dar es Salaam jana.



Na Asia Mbwana

BAADA ya Tanzania kujikuta ikishindwa michezo mingi ya kimataifa, hatimaye sasa imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Dunia wa kuruka kamba Olarndo nchini Marekani.Tanzania imenyakua ubingwa huo baada ya mchezaji wake, Hamisi Kondo kushinda 'Doble Check' na 'Consecutive Triple unders' katika mchezo imejinyakulia ubingwa wa dunia katika mchezo wa kuruka kamba nchini Marekani, kwa mchezo unaojulikana kama 'Double Check' na 'Consecutive triple unders'.


Kondo ambaye alikuwa akilelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Dogodogo Centre kilichopo Kigogo Dar es Salaam alipata ubingwa huo baada ya kushika nafasi ya pili katika mchezo wa Double check, huku Consecutive akishika nafasi ya tatu.Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kituo cha Mafunzo ya Michezo cha Tanzania Sport Training Centre (TSTC), Dennis Makoi alisema watu wasibague michezo ya kuruka kamba, kwani ni sawa na michezo mingine.

"Tusibaki kung'ang'ania michezo mingine na tuupe kipaumbele mchezo wa kamba kama tuipavyo michezo mingine," alisema.Aliishukuru Serikali ya Tanzania na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ushirikiano w a l i o u t o a mpaka kuweza kufanikiwa kumpeleka kijana huyo katika mashindano hayo.

Makoi alizitaja nchi zilizoshiriki michuano hiyo mbali na Tanzania ni Kenya, Afrika Kusini, Marekani, Canada, Brazil, Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Trinidad na Tobago.


No comments:

Post a Comment