30 July 2013

WAZIRI MKUU THAILAND KUWASILI LEODavid John na Penina Malundo
WAZIRI Mkuu wa Serikali wa Thailand, Yingluck Shinawatra, anatarajia kuwasili nchini leo kwa ziara ya kikazi ambapo atapokelewa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete, katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumza Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik, alisema Waziri huyo ambaye atawasili jijini saa 6.30 mchana atapokelewa na kukagua gwaride maalumu na baadaye atasaini mikataba mbalimbali kati ya Serikali yake na Tanzania.
Sadik alisema ujio wa waziri huyo utasababisha baadhi ya barabara kufungwa na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu na kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo.
" Tu n awa omb a r a d h i wananchi kwa usumbufu utakaojitokeza kwani baadhi ya barabara zitatakiwa kufungwa kwa muda ili kupisha msafara wa kiongozi huyo na barabara hizo Nyerere, Railway Gerezani,Sokoine Drive hadi Ikulu."alisema
Aliongeza kuwa barabara hizo zitafungwa kuazia muda wa saa 6.00 mchana hadi 7.30 na katika kipindi hicho chote wananchi wanatakiwa kuwa wastamilivu na kufuata maelekezo watakayokuwa wanapewa na Polisi hasa kwa madereva.
Sadik aliongeza kuwa katika kipindi chote atakachokuwa hapa nchini atapata fursa ya kutembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti kwa siku moja na baadaye atarejea mjini Dar es Salaam.  

No comments:

Post a Comment