Na
Daud Magesa, Mwanza
MWENYEKITI wa
Msikiti wa Khoja Ithina Asheri, Mkoa wa Mwanza, Sibtain Meghjee amewataka
waumini wa madhehebu mbalimbali ya Dini nchini, kujenga utamaduni wa kusoma,
kujifunza mambo mazuri na kutunza aya za vitabu vya imani ya dini zao ili
kuondoa uhasama na tofauti za kidini katika kujenga taifa lenye mshikamano.
Alisema waumini
wa dini zote wanapaswa kujifunza vitabu vyao na vya dini nyingine na kuchukua
mazuri yaliyomo kwa ajili ya jamii sababu hakuna sehemu yoyote katika vitabu
hivyo iliyokashifu dini nyingine.
Meghjee alitoa
rai hiyo mwishoni mwa wiki wakati wa kongamano la kuhifadhi Quran lililofanyika
kwenye uwanja wa shule ya msingi Mbugani jijini Mwanza.
Alisema
Watanzania kutokana na imani tofauti ni vema wakajenga utamaduni wa kusoma
vitabu vya dini zao na kuhifadhi ujumbe mzuri uliomo kwa manufaa ya jamii.
Meghjee alieleza kuwa waumini
wakisoma vitabu vya dini zao na kusambaza ujumbe mzuri kwa jamii hakuna mahali
Watanzania watahasimiana kwa misingi ya kukashifu dini nyingine.
"Kongamano hili limeandaliwa
kutoa ujumbe mzuri kwa jamii ili kuondoa uhasama ulioibuka nchini kati ya
waumini wa dini na dini kutokana na baadhi kutoa matusi yanayokashifu dini
zingine," alisema.
Alisema taifa limekumbwa na mambo
yanayotishia amani na ustawi wa wananchi wake ambao wameishi miaka mingi kama
ndugu,lakini upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu kushindwa kusoma na
kuhifadhi ujumbe mzuri wa vitabu vya dini unasababisha kuwepo kwa uhasama kati
ya waumini wa dini moja na nyingine.
Meghjee alieleza katika kongamano
hilo, walialika waumini wa dini mbalimbali kuja kushuhudia na kujifunza jinsi
gani muumini anaweza kuhifadhi ujumbe uliomo katika vitabu vya dini yake kisha
akausambaza kwa jamii iweze kujifunza.
"Tumefanya hivi maeneo mengi
ya nchi yetu na mwitikio umekuwa mzuri, nia na lengo letu ni kuhamasisha
waumini wa dini nyingine wasome vitabu vyao ikiwezekana na vya dini zingine ili
wachukue mazuri na kuyasambaza kwa jamii.Tukifanya hivi tutaondokana na uhasama
na mambo yanayotishia amani, ustawi wa dini zetu na taifa," alisema.
Katika kongamamno hilo, Mohamed
Takihan (16) mwanafunzi wa masuala ya dini nchini Iran,alionesha umahiri wa
kutunza aya mbalimbali za Quran Tukufu ambapo alijibu maswali aliyoulizwa
kupitia kitabu hicho.
Takiihan ambaye ni
yatima, alianza kuhifadhi aya mbalimbali za Quran akiwa na umri wa miaka 10 na
bado angali anafanya hivyo amefanya hivyo mara hamsini
No comments:
Post a Comment