WA N A N C H I Wi l a y a n i Mbulu,hususan wa kata ya
Bashay Mkoani Manyara wamehimizwa kulima kilimo cha biashara zaidi ili
kubadilisha mazingira waliyonayo, anaripoti Mary Margwe, Mbulu.
Hayo yalibainishwa jana na Mkuu wa Wilaya hiyo
Bw.Anatory Choya wakati alipokuWa akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha
wadau wakati akizindua programu ya miundombinu ya masoko na uongezaji wa
thamani ya mazao na kuboresha asasi ndogo za kifedha Vijijini.
Alisema kuwa ni vizuri wananchi wanaotegemea zaidi
kilimo cha zao la vitunguu swaumu kujipatia kipato wakalima kilimo cha
kibiashara zaidi ili kuweza kubadiLisha mazingira waliyonayo sasa.
Bw.Choya alisema wananchi wa kata ya Bashay wamekua na
mafanikio ya kupata kipato kikubwa kutokana ulimaji wa zao la vitunguu ambapo
vinauzwa zaidi ndani na nje ya nchi ambalo linawasaidia kuendesha maisha yao.
Aidha, alifafanua kuwa licha ya kipato wanachopata
wakulima hao lakini wamekua wakijiingiza kwenye migogoro isiyo ya lazima mara
wavunapo zao hilo na kupata fedha,ikiwa ni pamoja na kuuza ng’ombe.
Aidha, kufuatia mradi huo unaopelekwa wilayani hapo
Mkuu huyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanathamini miradi mbalimbali
inayopelekwa na Serikali pamoja na asasi mbalimbali kuhakikisha wanaitunza ili
iweze kuwa endelevu na hatimaye kuweza kuwaletea mafanikio
Naye Afisa Kiungo wa Mradi wa Uongezaji wa thamani ya
mazao na kuboresha Asasi Ndodondogo za Kifedha Vijijini (MIVARF) wa wilaya hiyo
Bw. Gilba Constantino ,alisema Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika
la Kitaifa la kusaidia Maendeleo Kilimo (IFAD) na Benki ya Maendeleo Afrika
(AFDB), wanatekeleza programu ya miundombinu ya masoko ,ongezeko la thamani ,
na huduma za kifedha Vijijini(MIVARF).
Bw. Constantino alisema mpango huo ni wa miaka
saba,ambo ulianza 2011-2017,mpango uliotokana na mradi uliotangulia
‘Agricultural Marketing Systems Development Programme (AMSDP) and Rural
Finance’,na kusema kuwa lengo la mradi huo kupunguza umaskini kuongeza kasi ya
maendeleo kiuchumi endelevu ikienda sambamba na malengo ya Kitaifa ya maendeleo
kama Mkukuta/ Mkuza ,ASDP,ATI KILIMOKWANZA NA SAGGIT.
Aidha, alifafanua kuwa mradi huo una nia ya
kuziwezesha kaya za wazalishaji kuongeza kipato na kuwa na uhakika wa
chakula,ikiwa ni sambamba na kuwaunganisha wazalishaji hao na masoko,kuongeza
thamani ya mazao na masoko ya mitaji kupitia asasi ndogo za kifedha Vijijini.
"Katika mradi huu wanufaika ama walengwa ni
wazalishaji wadogo wasindikaji ,vikundi vya masoko,asasi ndogo za kifedha kama
vile saccos,vikundi vya kuwekeza na kukopeshana, vicobasilc, ambapo alifafanua
kuwa wanufaika wanategemewa kuongeza kipato na kuinua uchumi kwa
ujumla,kuongeza ubora katika uzalishaji ili kupata bei nzuri ya mazao,kuwa na
uhakika wa chakula,kuongeza uzalishaji wa mazao, kupunguza gharama za
uzalishaji.
No comments:
Post a Comment