Na Kassim Mahege
WATANZANIA wameshauriwa kulipa kodi kwa
wakati ili kuharakisha maendeleo ya taifa pamoja na kuepusha usumbufu wa foleni
dhidi yao.
Akizungumza na gazeti hili jana kwenye
maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam, Ofisa
Mwandamizi kwa Elimu ya Walipakodi Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Msafiri
Mbibo alisema hiyo ni mojawapo ya changamoto wanazokumbana nazo.
"Kuna malalamiko mengi ikiwemo suala
la msongamano wa watu wengi wanaposubiri kipindi cha mwisho cha kulipa kodi,
ambapo kunakuwa na msongamano wa watu wengi na kusababisha usumbufu kwao,"
alisema.
Alisema, ni vyema kutosubiri kipindi cha
mwisho kulipa kodi kwani wakati huo watu wengi huwa wanalipia, hivyo
kusababisha kero.
Akifafanua
zaidi alisema, TRA kazi zake kubwa ni kukadiria kiasi cha kulipakodi, kukusanya
kodi ikiwemo kuwasilisha makusanyo ya walipa kodi kwa Serikali.
No comments:
Post a Comment