02 July 2013

WATANZANIA ONGEZENI UBUNIFU - MSWATI III


 Fatuma Mshamu na Josephine Burton

MKAZ I wa Ki b a h a Kongowe aliyetambulika kwa jina la Albert Madeje (30) amefariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati akivuka barabara.
Tukio hilo lilitokea Juni 30, mwaka huu majira ya saa tatu kamili usiku alipokuwa akivuka barabara ya Morogoro eneo la Mbezi Mwisho.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura alisema ajali hiyo ilihusisha gari namba aina ya BWM iliyokuwa ikiendeshwa na Herman Berege.

Kamanda huyo alisema, dereva huyo alikuwa akitokea Mbezi kwa Yusuph akielekea Kimara.
Alisema, alipofika maeneo hayo alimgonga mwenda kwa miguu huyo aliyekuwa akivuka barabara.
Katika ajali hiyo, Wambura alisema, Albert alifariki papo hapo.
"Baada ya kutokea ajali hiyo madereva wa bodaboda wa eneo hilo walijichukulia sheria mkononi na kumshambulia dereva huyo.
"Kwa kumpiga mawe, fimbo na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili na kuharibu gari lake kwa kulivunja vioo kwa mawe na kumpora mali alizokuwa nazo kwenye gari," alisema.
Hata hivyo, Kamanda huyo alisema maiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na dereva amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo hakuna aliyekamatwa na upelelezi unaendelea.

No comments:

Post a Comment